Photobucket

Friday, September 16, 2011

MOTO WAZIBITIWA KIDUCHU MBEYA SOKONI, POLISI WAFYATUA MABOMU YA MACHOZI KUWEKA USALAMA

 Na Keneth Goliama
MABOMU yatumika kuwatawanya wananchi waliokuwa wakimiminika katika Soko la  SIDO mkoa wa mbeya kwa ajili ya kusaidia kuuzima huku baadhi ya vibakla  wakimiminika kuiba bidhaa katika soko hilo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kutumia mabomu ya machozi kuweza kuwasambaratisha wananchi hao.

 hatua hito ilifanya wanachi kusambaratika na Jeshi la Polisi kuweza kuweka ulinzi mkali kwa  baadhi ya amaduka  ambayo hayakufikiwa na moto huo.

lichaa ya kusababisha hasara kubwa kwa wananchi wengi sana hapa mkoani Mbeya hasa katika tukio la kuungua masoko, wananchi bado wanahofu kubwa kuwa hii ni kuhujumu wafanya    biashara ambao ni wananchi wa mkoani hapo. Mkuu wa mkoa Mpya wa Mbeya (picha library)

Wakiongea kwanyakati tofauti wananchi hao walisema kwanini kila baada ya miezi sita ajali za moto ni katika masoko ya jiji la Mbeya tu na isiwe sehemu nyingine na ikizingatikwa kuwa ndio kitovu kikuu cha  biashara mkoani hapa.
Walisema hapa   lazima kuunda tumne nzito ya kuchunguza tatizo hilo na sio kutegemea ripoti zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa yanakuwa hayana ukweli mkubwa hii ni kutokana  na baadhi ya tume mbalimbali zikiwa zinashindwa kutoa jibu la kuwaridhisha wananachi.
 MOTO ukiwa umeteketeza kila kitu katika  baadhi ya maeneo huku zima moto zikiwa hoi kuuzima moto huo

 POLENI: wafanyabiashara wa Mkoa wa Mbeya  hawapo Pichani wakishuhudia  maduka yao yakiwa yanateketea kwa moto
Wafanya biashara na wanachi wakiangalia kuteketea kwa baadhi ndani ya soko la SIDO mwanjelwa Mkoani Mbeya huku wafanyabiashara hao wakihanishwa mda wa miaka miwili iliyopita kwa kuunguliwa na soko.  (Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu)

MOTO WATEKETEZA SOKO JIPYA LA SIDO- MWANJELWA-MBEYA


Na keneth Goliama.
SOKO la sido- mwanjelwa  jijini Mbeya linateketea kwa moto baada ya  kusadikikika kutokea kwa shoti ya umeme majira ya saa tatu na kusababisha moshi mzito katika soko hilo, huku wafanyabishara na wananchi wakiwa katika  hali tete kutokana na janga hilo kujitokeza kila baada ya m mwaka

Friday, September 9, 2011

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA WIKI HII TANESCO

 Hitimisho ya Ziara ya waziri wa Nishati na Madini  Mh. Wiliamu Ngaleja kwa waandishi wa habari na kuwasihi kuwa watanzania wataepukana na Mhao wa Umeme kwa siku za hivi karibuni.

 KARIBU:  Mh. Wiliam Ngeleja akifika katika ofisi za TANESCO kwa ajili ya kuanza ziara ya ukaguzi wa mitambo ya umeme wa dharura.

  Waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata habari katika mitambo ya  Jacobsen  eneo la Ubungo ,Dar Es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Wiliam Mhando akitoa maelezo kwa  waandishi wa Habari kuhusu upatikanaji wa umeme  hapa nchini.

MITAMBO YA JACOBSEN IKIFANYA KAZI


Mitambo ya Symbion ikiwa katika kuhakikisha mgao wa umeme unaendelea kuwa katika hali ya kawaida hapa nchini , mitambo hii inauwezo wa  kuzalisha umeme wa Megawatt 112

Vifaa vya mtambo wa Jacobseni ikiwa katika harakati za kufungwa ili kuweza kuzalisha umeme wa megawatt 100. mitambo hii imekodiwa kutoka finland kwa msaada wa serikali.

ZIARA YA MH. WILIAM NGELEJA KATIKA MITAMBO YA KUFUFUA UMEME WA DHARURA

Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja akielekezwa jinsi ya kuvaa kofia kabra ya kuingia kwenye mitambo kwa ajili ya ukaguzi wa muendelezo wa mafundi katika kuhakikisha mgawo unatoweka nchini. kutoka kulia ni Kaimu katibu mkuu wa wizara Eliakimu Maswi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Wiliam Mhando.





 Eng Moses Mwandenga Manager mitambo Symbion akitowa maelezo kwa waziri Ngeleja jinsi mafuta yanavyo sambaa kutoka kwenye matanki  kuelekea kwenye mitambo ili kuweza kuzalisha umeme. by Keneth Goliama

LIGI MBEYA KUANZA KURINDIMA BAADA YA MDHAMINI KUJITOKEZA



Keneth Goliama.

JIJI la Mbeya litazindua michezo  kwa vijana  ili kuweza kuinua vipaji vya wachezaji baada ya kujitokeza mdamini  wa kuendesha soka  .
Hayo yalisemwa na  chama cha mpira mkoani Mbeya (MUFA) kuwa  kandanda la mkoa wa mbeya linatarajia kuanza septemba 17 ambapo timu zaidi ya kumi na tatu zitaingia katika  mashindano hayo.
Mwenyekiti wa MUFA John Gndwe alisema  kampuni ithapa kuwa watanzania hasa katika mkoa wa Mbeya wataanza kushuhudia kandanda baadaya ya mdamini kupatikana .
Gondwe alimtaja mdhamini huyo kuwa ni A ccessories Coputer  LTD (ACL) ambaye atakuwa mdhamini mkuu wa kandanda mkoani hapa.
 Aliwasihi wachezaji kujituma katika timu zao ili kuweza kuongeza katika michezo  na vipaji zaidi  ili kurudisha hadhi ya jiji kwa kuwa  ndio lililosifiwa kwa ubora wa soka.
Alisema kuuwa mshindi wa kwanza atazawadiwa kitita cha shilingi 300,000  na mshindi wa pili atajinyakulia shilingi 150,000 na  mshindi wa tatu atajichukulia shilingi100,000
Gondwe alisema tumu zinazotarajia kuingia katika kinyang`anyilo hicho ni Zaragoza FC, Black scorpion ,Air port Rangers, Ilemi shooting star , eleven boys, winners FC,Ilomba town Stars ,Uyole Stars , Iyunga stars na Vijana FC.

Thursday, September 8, 2011

WANANCHI WALIOMBA JESHI LA POLISI RADHI MKOANI MBEYA

Na Keneth Goliama,Mbeya.

WANANCHI katika kijiji cha Inyala  Mbeya Vijijini  wameliomba jeshi la polisi radhi kwa li kufuatia vurugu zilizoibuka Agost 28 mwaka  kwa kufanya vurugu katika  kituo cha polisi na kutaka kukichoma moto na  kupanga mawe barabarani kwa lengo la kushinikiza wenzao waachiwe huru.

Akiomba radhi kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho Afisa Mtendaji wa Kijiji  Yusufu Abdala  kwa  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Evansi Balama  alisema alisema kufuatia vurugu hizo wameiomba serikali iwasamehe kutokana na kutofahamu taratibu na sheria zinazo kataza kufanya maandamao bila kufuata taratibu na sheria zilizopo kwa baadhi ya wananchi ho mkoani Mbeya.

 A
lisema  wakazi wa kijiji hicho  walivamia  eneo la kituo cha polisi kwa lengo la kutaka wenzao waachiwe huru kutokana na kufanya kosa la kushiriki kuua wezi waliotaka kuiba katika kijiji hicho kuwa kupinga kukamatwa wenzao wawili waliojeruhiwa kwa kuchomwa kisu na kupigwa nondo na mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mwizi ambaye baadaye aliuwawa na wanakijiji.

Mtendaji huyo alissema ni kweli kabisa wanankijiji wanaomba radhi kwa kufanya vurugu lakini ukweli ni kwamba wananchi wasingeweza kuvumilia hasira walizokuwa nazo za kukamatwa kwa wananchi wenzake ambao wanahusishwa na tukio hilo.

Alisema kitendo cha mtu huyo kuvamia kijijini hapo na kuvunja duka la mfanyabiashara mmoja kijijini hapo na kupora vitu mbalimabali ndio sababu ya  wananchi kupandwa na hasira na kuanza kuwafukuzawezi hao na kuwakamana na kuwauwa

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Mbeya alisema  ni kosa wananchi kujichukulia hatua  mikononi na kuwasihi kuchukua sheria na kuwapeleka katika vyombo husika ili sheria iweze kufanya kazi yake na kuwasihi huo ndio utawala bora