Photobucket

Thursday, September 8, 2011

WANANCHI WALIOMBA JESHI LA POLISI RADHI MKOANI MBEYA

Na Keneth Goliama,Mbeya.

WANANCHI katika kijiji cha Inyala  Mbeya Vijijini  wameliomba jeshi la polisi radhi kwa li kufuatia vurugu zilizoibuka Agost 28 mwaka  kwa kufanya vurugu katika  kituo cha polisi na kutaka kukichoma moto na  kupanga mawe barabarani kwa lengo la kushinikiza wenzao waachiwe huru.

Akiomba radhi kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho Afisa Mtendaji wa Kijiji  Yusufu Abdala  kwa  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Evansi Balama  alisema alisema kufuatia vurugu hizo wameiomba serikali iwasamehe kutokana na kutofahamu taratibu na sheria zinazo kataza kufanya maandamao bila kufuata taratibu na sheria zilizopo kwa baadhi ya wananchi ho mkoani Mbeya.

 A
lisema  wakazi wa kijiji hicho  walivamia  eneo la kituo cha polisi kwa lengo la kutaka wenzao waachiwe huru kutokana na kufanya kosa la kushiriki kuua wezi waliotaka kuiba katika kijiji hicho kuwa kupinga kukamatwa wenzao wawili waliojeruhiwa kwa kuchomwa kisu na kupigwa nondo na mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mwizi ambaye baadaye aliuwawa na wanakijiji.

Mtendaji huyo alissema ni kweli kabisa wanankijiji wanaomba radhi kwa kufanya vurugu lakini ukweli ni kwamba wananchi wasingeweza kuvumilia hasira walizokuwa nazo za kukamatwa kwa wananchi wenzake ambao wanahusishwa na tukio hilo.

Alisema kitendo cha mtu huyo kuvamia kijijini hapo na kuvunja duka la mfanyabiashara mmoja kijijini hapo na kupora vitu mbalimabali ndio sababu ya  wananchi kupandwa na hasira na kuanza kuwafukuzawezi hao na kuwakamana na kuwauwa

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Mbeya alisema  ni kosa wananchi kujichukulia hatua  mikononi na kuwasihi kuchukua sheria na kuwapeleka katika vyombo husika ili sheria iweze kufanya kazi yake na kuwasihi huo ndio utawala bora

No comments:

Post a Comment