Photobucket

Friday, September 9, 2011

LIGI MBEYA KUANZA KURINDIMA BAADA YA MDHAMINI KUJITOKEZA



Keneth Goliama.

JIJI la Mbeya litazindua michezo  kwa vijana  ili kuweza kuinua vipaji vya wachezaji baada ya kujitokeza mdamini  wa kuendesha soka  .
Hayo yalisemwa na  chama cha mpira mkoani Mbeya (MUFA) kuwa  kandanda la mkoa wa mbeya linatarajia kuanza septemba 17 ambapo timu zaidi ya kumi na tatu zitaingia katika  mashindano hayo.
Mwenyekiti wa MUFA John Gndwe alisema  kampuni ithapa kuwa watanzania hasa katika mkoa wa Mbeya wataanza kushuhudia kandanda baadaya ya mdamini kupatikana .
Gondwe alimtaja mdhamini huyo kuwa ni A ccessories Coputer  LTD (ACL) ambaye atakuwa mdhamini mkuu wa kandanda mkoani hapa.
 Aliwasihi wachezaji kujituma katika timu zao ili kuweza kuongeza katika michezo  na vipaji zaidi  ili kurudisha hadhi ya jiji kwa kuwa  ndio lililosifiwa kwa ubora wa soka.
Alisema kuuwa mshindi wa kwanza atazawadiwa kitita cha shilingi 300,000  na mshindi wa pili atajinyakulia shilingi 150,000 na  mshindi wa tatu atajichukulia shilingi100,000
Gondwe alisema tumu zinazotarajia kuingia katika kinyang`anyilo hicho ni Zaragoza FC, Black scorpion ,Air port Rangers, Ilemi shooting star , eleven boys, winners FC,Ilomba town Stars ,Uyole Stars , Iyunga stars na Vijana FC.

No comments:

Post a Comment