Photobucket

Friday, September 16, 2011

MOTO WAZIBITIWA KIDUCHU MBEYA SOKONI, POLISI WAFYATUA MABOMU YA MACHOZI KUWEKA USALAMA

 Na Keneth Goliama
MABOMU yatumika kuwatawanya wananchi waliokuwa wakimiminika katika Soko la  SIDO mkoa wa mbeya kwa ajili ya kusaidia kuuzima huku baadhi ya vibakla  wakimiminika kuiba bidhaa katika soko hilo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kutumia mabomu ya machozi kuweza kuwasambaratisha wananchi hao.

 hatua hito ilifanya wanachi kusambaratika na Jeshi la Polisi kuweza kuweka ulinzi mkali kwa  baadhi ya amaduka  ambayo hayakufikiwa na moto huo.

lichaa ya kusababisha hasara kubwa kwa wananchi wengi sana hapa mkoani Mbeya hasa katika tukio la kuungua masoko, wananchi bado wanahofu kubwa kuwa hii ni kuhujumu wafanya    biashara ambao ni wananchi wa mkoani hapo. Mkuu wa mkoa Mpya wa Mbeya (picha library)

Wakiongea kwanyakati tofauti wananchi hao walisema kwanini kila baada ya miezi sita ajali za moto ni katika masoko ya jiji la Mbeya tu na isiwe sehemu nyingine na ikizingatikwa kuwa ndio kitovu kikuu cha  biashara mkoani hapa.
Walisema hapa   lazima kuunda tumne nzito ya kuchunguza tatizo hilo na sio kutegemea ripoti zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa yanakuwa hayana ukweli mkubwa hii ni kutokana  na baadhi ya tume mbalimbali zikiwa zinashindwa kutoa jibu la kuwaridhisha wananachi.
 MOTO ukiwa umeteketeza kila kitu katika  baadhi ya maeneo huku zima moto zikiwa hoi kuuzima moto huo

 POLENI: wafanyabiashara wa Mkoa wa Mbeya  hawapo Pichani wakishuhudia  maduka yao yakiwa yanateketea kwa moto
Wafanya biashara na wanachi wakiangalia kuteketea kwa baadhi ndani ya soko la SIDO mwanjelwa Mkoani Mbeya huku wafanyabiashara hao wakihanishwa mda wa miaka miwili iliyopita kwa kuunguliwa na soko.  (Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu)

No comments:

Post a Comment