MBUNGE wa mbeya mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) Joseph Mbilinyi kufanya ziara ya kikazi katika kata ya Iyunga ili kuweza kusikiliza kero za wananachi
Akiongea na Leotanzania Blogspot alisema katika ziara yake atafanya mikutano mbalimbali ili kuweza kusikiliza kero za wananchi na kuweza kufanyia ufumbuzi wa kero hizo
Baada ya kuahirishwa kesi yake anatarajia kufika katika kata hizo ili kuweza kuangalia matukio mbbalimabali na kuweza kujionea maendeleo ndani ya kata hiyo pamoja n akufanya kazi nao.
Kabla ya kuondoka katika mahakama alisema huu umati uliopo hapa ni kusikiliza jisi gani mwenendo wa kesi unavyoelekea ili kuweza kumpa moyo katika tatizo hilo.
Alisema wananchi wanaodai fidia baada ya Serikali kuchukua maeneo yao kwa ajili ya upanuzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) wameniambia hivyo ni wajibu wake kufika na kusikiliza matatizo yake ili kuweza kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.
“Nategemea kukutana na wananchi wa Iyunga ili kuweza kujua matatizo yao nini ili kuweza kuleta ufanisi mkubwa katika kata hiyo bila kufanya itikadi maana haya ni maendeleo ya jiji letu “ alisema Sugu.
No comments:
Post a Comment