Na keneth Goliama
Mgombea ubunge jimbo la Mbeya mjini maarufu kwa jina la Sugu amekuwa kivutio kwa siku mbili mfulululizo katika midahalo ya wagombea inayoendeshwa na shirika la utangazaji Tanzania (TBC1) na wa MBENGONET kwa kushirikiana na jumuiko la taasisi za kiraia Tanzania.
Mbilinyi amekuwa akivutia katika midahari hiyo ambayo ilihusisha wagombea ubunge watatu wa jimbo la Mbeya mjini kutoka katika vyama vya Demokratic Party(DP),ambapo kinawakilishwa na Alimu Tokolosi Sulauli,chama cha wananchi( Cuf ) kinachowakilishwa na Prince Mwaihojo na Chama cha Demokrasia maendeleo Chadema ambacho kinawakilishwa na Joseph Mbilinyi (SUGU)
Katika midahalo hiyo ambapo wa kwanza uliendeshwa na taasisi ya MBENGONET ulifanyika jana (juzi) katika ukumbi wa Benjamini mkapa uliopo Soko matola jijini Mbeya ambao ulikusanya umati mkubwa watu waliooyesha wazi kumkubali Mbilinyi kwa kumshangilia mwanzo hadi mwisho wa mdahalo na kumzonga kwa kumsindikiza hadi kwenye gari yake.
Hali ya kuwa kivutio sugu haikuishia hapo bali iliendelea hadi katika mdahalo uliofanyika leo (jana) katika ukumbi wa dhandhoo ulioandaliwa na shirika la utangazaji (TBC1) ambapo nyotake iliyoonyesha kung`ara mwanzo wa mdahalo hadi mwisho na kila mara alipotakiwa kujibu maswali ya wananchi waliohudhuria katika mdahalo huo.
Akizungumza katika mdahalo huo Mbilinyi alisema kuwa endapo kama atachaguiwa kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini ataishauri Serikali kurudisha utaratibu wa zamani uwekaji wa bomba za maji kila mtaa ili kuzogeza karibu huduma za maji kwa wananchi ambao hawana uwezo kuvuta maji ndani ya nyumba zao.
“Endapo kama nitachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini ni taishauri serikali kurudisha utaratibu wa uliokuwepo enzi za Mwalimu Jullius Kambgarage Nyerere wa kuweka bomba kila mtaa kwa ajili ya kusogeza huduma za maji karibu kwa waanachi ambao hawana uwezo wa kuingiza maji ndani”alisema
Alisema kuwa kwa sasa kumekuwepo na tatizo kubwa la maji ambapo wananchi ambao hawana uwezo wa kuingiza maji katika nyumba zao wanaangaika siku nzima kusaka maji na wakati mwingine kununua maji kwa wale wenye uwezo ambao wameweka maji ndani utaratibu ambao pia unakatazwa na idara husika zinazosimamia maji hayo.
Mbilinyi alisema kuwa katika kuzunguka kwake katika jimbo la Mbeya mjini amekuta katika maeneo mengine amekuta kuna vipisi vya mabomba lakini havoti maji na kusababisha wananchi wengi kukosa huduma ya maji ya bomba.
MWISHO
No comments:
Post a Comment