NaKeneth Goliama
HALMASHAURI ya jiji la Mbeya inatarajia kuuunda kamati maalum itakayozunguka maeneo ya masoko na vilabu vya pombe za kienyeji kwa ajili ya kuwasaka watoto ambao wameacha shule na kuamua kufanya vibarua
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mbeya Iddi Juma ali[okuwaakizunumza na waandishi wa habari na wanachama wa chama cha waandishi wa habari za Ukimwi Tanzania (AJAAT) waliokuwa wakifanya ziara ya kufuatilia agenda ya watoto na kuibua matatizo yanayowakabili kwa hisani ya shirika la watoto Duniani (UNICEF)
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kutokana na taarifa alizozipata kutoka kwa waandishi hao kuwa katika ziara yao wamebaini kuna watoto wengi wenye umri kuanzia miaka tisa hadi 14 wanatumikishwa katika maeneo ya masoko na vilabu huku wenzao wakiwa shuleni.
“Kwanza naoenda niwashukuru kwa niletea taarifa hizi kwani mi9mi hapa ni mgeni nina miezi miwili nimehamia kutoka Moshi hivyo nimezipokea taarifa hizi na inasikitisha kuona kuwa kuna watoto ambao hawasomi shule na wanatumikishwa katika vilabu vya pombe za kienyeji na kwenye masoko huku wenzao wakati huo wakiwa madarasani”alisema
Alisema katika kuhakikisha tatizo hilo linapungua au kuondoka kabisa alisema kuwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kamati ya ulinzi na usalama na idara ya maendelepo ya jamii ataunda kamati maalum ambayo itazunguka maeneo hayo na kufanya utafiti wa kina ili kuweza kubaini ukubwa wa tatizo.
Aidha alisema kuwa ili kukomesha tabia ya kutumisha watoto wadogo halmashauri yake kupitia vikao vyake itaunda sheria ndogo ya kuzuia tabia hiyo ili mtu yoyote atakayebainika kuwa anahusika na tabia ya kutumikisha watoto wadogo achakuliwe hatua za kisheria .
Juma alisema kuwa pia wazazi wanajukumu kubwa katika kuwafuatilia watoto wao wawapo shuleni na nyumbai ili kuweza kusaidia hali hiyo isijitokeze kwani watoto wengine ambao wanafnya mambo hayo wanawazazi wao ambao hawajali maendeleo ya watoto wao.
Alisema kuwa hata hivyo halshauri hiyo itaandaa utaratibu wa kuhamsisha wazazi kuwa karibu na watoto wao ikiwa ni pamoja kuziongezea nguvu kamati za shule ili ziweze kufuwa karibu na wazazi hao kwa kuwafuatilina na kuwachukuliwa hatua endapo kama watoto wao hawafiki shuleni bila sababu yoyote ya msingi.
Mkurugenzi huyo aliwataka waandishi wa habari kuendelea kuisaidia serikali kuibua matatizo mbali mbali yanayowahusu watoto ambayo yamejificha na kuyafikisha sehemu husika ili kuweza kufanyiwa kazi na hivyo watoto kuweza kupata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na elimu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment