Na Keneth Goliama,Mbeya
MGOMBEA ubunge kupitia chama cha Demokrasia (DP) Alimu Tokolosi Suali aibukia kwenye mdahalo kitendo kilichofanya baadhi ya wananchi kushindwa kumjua kuwa ni mgombea kupitia chama gani kutokana na kutoanza kampeni zake.
Mgombea huyo aliyeibukia katika mdahalo ulioandaliwa na MBEGONET kwa kushirikiana na Jumuiko la Asasi za Kiraia Tanzania alisema uwezo wake ni mkubwa sana ndio maana hajazindua kampeni zake licha ya kubaki siku 20 kufanya uchaguzi.
Mgombea huyo aliyeibuka kwa kusema anahitaji wananchi kumchagua mgombea Urais DK Wilbroad Slaa ili aweze kushirikianannae katika kuhakikisha wanafumua mtandao wa mafisadi katika kuhakikisha wananchi wananeemeka na maliasili walizonapo hapa nchini.
“Ninaimani na Mgombea Urais wa Chadema DK. Wilbroad Slaa kwa ubora wake katika kazi kwa kuwa ni makini kwani ndie Rais pekee anayeweza kuimarisha Uchumi Huku wananchi waliofurika kusikiliza kushangilia sana” alisema Suali.
Suali ambaye ameibukia ukumbi wa mkapa kuhakikisha ananadi sera zake alisema si ajabu kumnadi kiongozi bora ambaye anaweza kuinua ubora wa wananchi wa Tanzania kwa kuwa huyu ni kiongozi makinik mwenye kuoneha umakini kulima maendeleo ya watanzania.
Alisema Tanzania ina migodi mingi ndio maana serikali imetenga mgodi wa Meremeta kwa kuwapa wizara ya Ulinzi (JWTZ) ndio chanzo cha jeshi hilo kuwa imara na kuhoji kwa nini Wizara ya elimu isitengewe mgodi wake wa Pekee ili kuhakikisha wananchi wanasoma bure.
Suali alisema ameamua kuanza kampeni zake za nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora ya kujua sera za wagombea ili atakapo ingia katika kampeni za majukwaani wananchi wengi wawe wanatambulika.
Alisema kipaumbele kikubwa ni kwa vijana kwa kuwa ndio chazo na nguvu mali za wananchi wa mkoa wa mbeya kwa kuimarisha vyua vya VETA, na kuweka sawa imani za kufufua vipaji wananchi.
Alisema Tanzania bila viongozi bora watanzania wataishia kulaumu wakati nafasi ni ya sasa kuchagua viongozi bora watakaoimarisha maendeleo ya nchi.
Mgombea huyo alionyesha nafasi yake kujitambulisha kwa wananchi na kuzishukuru taasisi zisizo za kiserikali kwa kuandaa na midahalo ambapo wagombea wasio na uwezo kutumia nafasi hizo katika kuhakikisha wanafikisha sera zao kwa wananchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment