Photobucket

Thursday, September 2, 2010

WANAFUNZI WAKUMBWA KWA USHIRIKINA MBEYA

Na Keneth Goliama,Mbeya.

WANAFUNZI zaidi ya 50 wateseka kwa imani ya kishirikina huku wengine wakiungua nguo walizovaa bila wao kuungua, kupatwa na kwikwi kitendo kinachafanya wanakijiji kutafuta mganga wa jadi kuja kuchunguza tatizo.

Wanafunzi hao wa shule ya sekondari ya Itala iliyoko Irambo ,Mbeya Vijijini wamekuwa wakikumbwa na tatizo hilo kwa mda wa miezi miwili bila ya kupatikana kwa tiba na kusababisha wanafunzi hao kushindwa kusoma.

Vyazo vya habari kutoka ndani ya shule Itala zinasema kuwa wanafunzi waliokataa tiba za jadi bado wamekuwa wakiendelea kuunguliwa nguo na wengine wakipatwa na kwikwi kitendo kinachohatarisha maisha ya wanafunzi hao.
Wanafunzi hao ambao wakitaka kwenda kusoma moto huwafuata nyuma yao na kusababisha kupiga kelele na wengine kuzimia kwa kile kinachoelezwa kuogopa kushikwa na imani za kishirikina.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Mbeya Evance Balama alikiri kupata taarifa kutoka shule ya Itala kwa kukumbwa na tatizo la kishirikina na kufika maramoja kuwaona wanafunzi hao wakiteseka.

Balama alisema baada ya kupewa taarifa na mkuu wa shule na maamuzi ya wanakijiji kumtafuta mganga wa Jadi kuja kuwatibu watoto hao hakuona tabu kwa maamuzi yao ila alisema kisheria serikali haitambui imani za kishirikina .

Alisema kwa kuwa zaidi ya watu 16 walikamatwa na kukiri kujihusisha kwa tendo hilo na wengine walijitokeza kwa kuweza kumleta mganga huyo kutoka Malawi ambaye walisema ndio mtatuzi wa janga hilo.

Barama alisema iwapo watamleta mganga wa jadi huyo lazima awe na vibali vya kuingia hapa nchini na ruhusa ya kutibu kwa njia ya jadi nakuwa iwapo watashindwa walete taarifa katika ofisi yake.

“Sitaki kusema na kujua kama kunaushirikina ila kwa kuwa waliniambia kuna mtu kutoka Malawi kuja kutatua tatizo hilo sio tabu bali afate sheria za uingiaji hapa nchini.” Alisema Barama

Aliongeza kuwa amekuwa akifika katika kijiji hicho kukemea ushirikina kutokana na matukio ya kishirikina yakiwa yanajitokeza kwaa wingi na hivyo kusababisha hata walimu kuogopa kwenda kufundisha shule hiyo kutokana na imani za kichawi.

No comments:

Post a Comment