WAKATI Chadema ikilalamikia ahadi za mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete kwamba zinakiuka Sheria ya Gharama ya Uchaguzi, mgombea huyo ameongeza ahadi nyingine kwamba, serikali yake itawagawia vyandarua wanaume wote nchini ili kupambana na malaria.
Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kwenye uwanja wa mpira wa sokoine wakati wamkutano kampeni ya kuwania urais kwa kuahidi kila nyumba itapewa vyandarua viwili ili kukomesha maralia.
Kikwete alisema kuwa wat wengi wamekuwa wakitumia vyandarua vya watoto vya kujikinga na maambukizi ya maralia vilivyotolewa bure na serikali kwa ajili ya kupunguza ugonjwa huo.
Alisema licha ya serikali kupulizia dawa nyumba kwa nyumba katika mikoa wa kigoma ili kuua wadudu wanaoambukiza maralia lakini bado kiasi cha uambukizaji kimekuwa kikubwa.
Kikwete alisema lengo la kugawa vyandarua kwa kila nyumba kitasaidia kukomesha maamubukizi ya maralia kwa sababu watu wote katika nyumba watatumia chandarua hata baba ndani ya nyuma atakitumia.
Alisema nchi ya Cuba imeweza kusaidia Tanazania kwa kiasi kikubwa kutokomeza maralia kutokana na janga hilo kutaka kuwa sugu ndio maana serikali imeamua kuchukua tahadhari kwa kiwango kikubwa.
“Tupambane na kukomesha maralia kwani nidio gonjwa linaloweza kuzuia kuliko ukimwi kwani ukimwi tunahamasisha watu kuacha kuliko maralia “ alisema Kikwete
Alisema jamii inatakiwa kujua kuwa maralia haikubaliki kwani ni gonjwa ambalo huuwa watu wengi na tukikataa maralia tutaweza kuitokomeza kabisa.
Aliongeza kuwa Licha ya serikali kutambua uhaba wa wataalamu hasa madakatari, kwa kushirikiana na vyuo vya tiba hapa nchini vitasaidia kuongeza wataalamu kuhakikisha maralia na magonjwa mengine yanapatiwa watalaamu.
Alisema Serikali kwa kushirikiana na KCMC ,Bugando ,Mhimbili, na kanisa la Wakatoriki vinafanya juhudi kubwa kuhakikisha watalaamu wanapatikana.
Pia alisema atahakikisha sehemu zaidi za kuweza kuwalaza wagongwa katika hospitali ya mkoa wa Mbeya zinajengwa ili kuboresha afya za wagonjwa na kutoa usumbufu unaojitokeza.
Mwisho
No comments:
Post a Comment