Photobucket

Monday, August 30, 2010

WAKULIMA WATAKA WAFUGAJI WAONDOLEWE CHUNYA

Na Keneth Goliama, Chunya.

WANANCHI walioharibiwa Hekta 75 za mahindi katika Bonde la Mwambani Wilayani Chunya wameomba serikali kuharakisha haraka kuwatoa wafugaji wa kisukuma walioko karibu na mashamba ili kuepusha migogoro baina yao.

Wakizungumza na mwananchi katika kata hiyo wakulima hao walisema wafugaji hao wamekuwa wakifanya jambo hilo kwa makusudi wakidai kuwa bonde hilo wamelinunuwa kwa viongozi wa serikali kwa ajili ya kulisha mifugo yao hivyo kuwaacha hapa ndio kusema wameshindwa kuwatoa.

Zainabu Hamis alisema kuwa kuwaacha wafugaji hawa ni kuonesha serikasli inawaogopa hivyo ili kuhakikisha amani inapatikana ni bora kuwaondoa kabisa katika bonde hilo kama ilivyofanyika bonde la Mbalali.

Alisema kuwa kipindi cha masika walishindwa kuvuna mazao yao kutokana na mvua nyingi iliyonyesha mwaka huu hivyo waliamua kulima tena kipindi hiki cha kiangazi na kwamba mazao yao yalikubalika sana alkini kutokana na wafugaji kuingia mara kwa mara ndani ya hilo kunawafanya kukosa kabisa chakula .

Alisema kuwa yeye hana tena chakula kwani alikuwa akitegemea mazao hayo ili alishe familia yake ambayo yameteketezwa na mifugo ya wasukuma ambao wamekuwa wakilisha mifugo yao usiku ambapo wange wanakuwa wamelala.

Wakulima hao waliodai kuwa wameshindwa kuwadhibiti wafugaji hao kwani licha ya kuweka faini ya pesa ya Shilingi 20000 ya kila ng`ombe lakini imekuwa ushuru wa kawaida kwa wafugaji hao wanapokamatwa kwani suala hilo limekuwa likishughulikiwa polepole.

Alisema kuwa malalamiko yao wamekuwa wakipeleka katika kituo cha Polisi cha Mkwajuni lakini alidai Polisi hao wanawaeleza kuwa waende na vithibitisho ambavyo ni Ng’ombe au Mtu jambo ambalo alisema ni vigumu kwao.

Alisema haiwezekani wao kukamata ngombe ya wasukuma kwani wanalisha mifugo hiyo usiku na kwamba wakifanya hivyo basi wataanzisha vita baina yao na wafugaji kwa kuwa wafugaji wakiona ng’ombe wao haonejani wanajiaanda na siraha kumsaka ng’ombe wao.

Kwa upande wake Mbakishe Mkinga alisema wanaowapa kiburi wafugaji ni viongozi wa juu akisema wao wanachukuwa pesa nyingi kwa wafugaji bila kuwaeleza wapi wakapeleke mifugo yao ndiyo maana wafugaji wanaendelea kuwanyanyasa kwa kuharibu mizao yao .

Walisema kuwa Mbale amekuwa akitengeneza pesa kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wafugaji, hivyo hao wasukuma hawawezi kuacha tabia ya kulisha ng’ombe mazao ya wakulima na kuongeza kuwa kauli mbiu ya kilimo kwanza kwao itakuwa ndoto licha ya kujitahidi kulima.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwambani Frank Mayale alisema kilio cha wakulima katika eneo hilo ni cha muda mlefu lakini jitihada za serikali kuwasaidia wakulima hao bado hazipo kwani licha kupoteza ekari za mahindi msada wa kuwaondoa wafugaji hao bado ni mdogo.

Alisema kuwa Afisa Mifugo ambaye ni Mbale anapofika usiku wafugaji wanaondoka lakini baada ya siku chache wanarudi tena kwa kuwa yeye anawalipisha pesa harafu na wao wanafanya hivyo kwa wakulima kama kuwakomoa.

Aliongeza kuwa baada ya kupata malalamiko mengi ya kuhalibika kwa mazao ya wakulima walipeleka malalamiko hayo kwa uongozi wa wilaya ambapo walisema wapeleke tathimini ya watu walioathirika na mifugo hiyo ambapo alisema hadi leo hii hawajapata majibu.

WAlisema licha ya serikali ya wilaya kupeleka watathimini imekuwa ni geresha tu kwao maana maofisa wa kilimo wanaotumwa ni walewale wanaolipisha pesa kwa wafugaji ndio maana wafugaji wanakuwa jeuri sana

Mwisho.

No comments:

Post a Comment