Na Keneth Goliama,Mbeya.
OFISI za Halimashauri ya jiji la Mbeya zawaka moto baada ya hitilafu ya umeme kutoka katika ukumbi wa mikutano majira ya asubuhi baada ya ofisi kufunguliwa.
Moto huo ulioanza majira ya saa 2:17 asubuhi uliwaka moto baada ya nyaya za umeme kusadikika kuchoka kutokana na jengo hilo kutofanyiwa ukarabati toka enzi za mkoloni kuwa zinaongezwa tu panapohitajika kuongezwa umeme.
Mashuhuda wa tukio hilo ambao ni wafanyakazi wa Halmashauri hiyo walisema kuwa mara ya kwanza walidhani umeme umekatika, lakini baada ya dakika chache walianza kuhisi harufu ya moshi wa kitu kama mpira ulioungua na ndipo wakatoka nje kujinusuru roho zao.
“tulitoka nje na ndipo wengine tukaamua kupiga simu kwa kikosi cha zimamoto kwani moshi mkubwa ulitanda jingo zima, baada ya dakika tano kikosi cha zimamoto kilifika na kuanza kufanya kazi ili kuudhibiti moto huo”.
Wafanyakazi hao walisema moto huo ulianzia darini ambapo vitu vingi viliungua ikiwamo viti nyaraka za ofisi ambazo hazikufahamika thamani yake.
Naye Gwatwa Lusajo mhudumu wa mstaiki meya alisema alipofika alisikia harufu ya kusadiki kuwa ni moto ndipo alipochukua funguo na kufungua aliona moshi mkali ndipo alipopiga kelele kuwaarifu wafanyakazi.
Hata hivyo gari la zimamoto lililokuwa na namba SM 4524 aina ya Mercedes Benz lilifika na kuanza kuzima ambapo Mkuu wa Kikosi hicho Sajenti Juma Mwale alisema wamepigiwa simu kwenda kuokoa mali za ofisi, tulifika baada ya dakika 20 kuzima moto na kufanikiwa kuuzima.
“sisi tulipigiwa simu na sajenti Sanga ambaye alituambia kuwa kuna moto unawaka hatukufanya mawasiliano yoyote na TANESCO tukaja kuzima tu na hakuna madhara yaliyojitokeza zaidi sana tumeokoa samani zote zilizokuwemo licha ya kuungua kwa kiasi”.
Kaimu MKurugenzi wa Jiji la Mbeya Dkt. Samuel Lazaro alikiri kuwa jengo la halmashauri hiyo ni la zamani “tangu enzi za mkoloni ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba hakuna madhara makubwa yaliyojitokeza.
Lazaro alisema madhara yaliyojitokeza ni kuungua kwa dari ya ukumbi wa mikutano ila mwaka wa fedha 2010/2011 kumetengwa fedha kwa ajili ya kulikarabati jingo lote na hususani katika mfumo wa umeme na ukarabati huo utachukua miezi takribani miwili”.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment