Wednesday, August 18, 2010
SERIKALI KUONGEZA RUZUKU
Na Keneth Goliama, Mbeya.
SERIKALI mkoani Mbeya imetoa ruzuku ya vocha 5200 za mbolea za ruzuku zenye thamani ya shilingi 120 ambazo zimegaramia mbolea hizo ili kuondokana na kero na kufanya serikali kutekeleza azma yake ya kutekeleza azma ya kilimo kwanza.
Akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa John Mwakipesile alieleza kuwa serikali imetoa ruzuku za mbolea hizo ili kuweza kupunguza tatizo la upungufu wa mbolea na kufanya kazi ya kuongeza uzalishaji huo.
Alisema serikali imeamua kutoa ruzuku hiyo kwa wilaya ya Mbeya vijijini na Mbeya mjini ili kuhakikisha ule upungufu wa mbolea unakwisha na kuhakikisha kuwa wanainchi wanapata mbolea hizo na kufanya zinatumika katika mda huu wa kilimo.
Mwakipesile alisema Mbolea hiyo itatumika katika kupandia na kukuzia ili kuhakikisha uzalishaji wa mazao unafikiwa kiwango kilichotarajiwa na kuvuka kiwango cha uzalishaji katika mkoa wa Mbeya na kufanya azma ya kilimo kwanza inavuka malengo.
Aliwaasa wanachi kutumia mvua zinazo nyesha kuhakikisha wanapanda msimu ujao ili kufikia malengo ya mkoa kwa kwa kuzalisha zaidi ya tani 4.4 milioni na ikiwezekana kuvuka malengo ya uzalishaji wa mwaka 2010.
Alisema kutokana na ongezeko la mbolea iliyotolewa na serikari kupelekwa kwa wananchi kutasaidia wananchi kuvuna mazao mengi ili kuweza kutumia katika maendeleo ya maisha yao.
Mwakipesile alisema kuwa mbolea hizo zitatumika katika wilaya ya Mbeya vijijini na Mbeya mjini kwani wao ndio wanakuwa na mvua nyingi na kupanda misimu miwili na kuwashauri wananchi kutumia kulima na kuitumia mboea ya ruzuku hiyo kuhakikisha wanaitumia vizuri.
Aliongeza pia kuwa hata mvumilia kiongozi yeyote amabaye ataitumia mbolea ya ruzuku kwa maslahi yao binafsi na sio kwa manufaa ya wananchi, mbolea hiyoaliyokuwa na mgawanyiko wa mbolea ya kukuzia na kupandia zilizogawanywa katika vocha 2600 kwa ajili ya kupandia nakukuzia vocha 2600.Mkoa wa Mbeya unatarajia kuvuna tani 4.4 milioni za mzao mbalimbali ambapo mkoa huo utakuwa umevuka malengo kutokana na kuongezeka kwa mbolea hizo.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment