Photobucket

Wednesday, August 18, 2010

WASHAURIWA KUFUGA KUKU WA KIENYEJI

Na Keneth Goliama,Mbeya.

Wananchi washauriwa kuongeza ufugaji wa kuku wa asili kwasababu kuku hao huzaliana kwa wingi ukilinganisha na kuku wa kisasa ,ambao hawatumii gharama kubwa katika kuwatunza pamoja na kujiunga katika vyama vya ushirika ilikupata mikopo.

Rai hiyo ilitolewa katika maonesho ya Nanenane naMkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile aliwashauri wananchi kujihusisha na ufugaji wa kuku wa asili pamoja kujiingiza katika vyama vya ushirika ili kuweza kupata mikopo kwa nia ya kuendeleza kilimo.

Mwakipesile alisema kuku wa asili huzaliana kwa wingi ukilinganisha na kuku wa kisasa kwakuwa kuku hao hutumia gharama kubwa katika kuwatunza ukilinganisha kuku wa asili.

“Naomba wakulima tumieni ujuzi muupatao katika ufugaji wa kuku wa asili kwa kuwa hauna gharama kubwa na unaweza kukupatia faida kubwa ukilinganisha kuku wa kisasa”alisema Mwakipesile.

Alisema kwakuzingatia nyenzo za kilimo bora na ufugaji wenye teknolojia ya kisasa unaweza kuinua kipato cha wananchi wa Tanzania kwa kufuga ng`ombe 2 milioni na Mbuzi 1.6 katika ya nyanda za juu kusini na kuwa kuku zaidi ya 5milion hupatikana.
Kwa kuwa serikali inatambua umhimu wa kuinua uchumi wa wananchi, wananchi wanatakiwa kujishughulisha na ufugaji wa kuku ili kuhakikisha wanainua maendeleo yao.

Pia alisisitiza kuwa wakulima wengi wakijiunga katika ushirika wanaweza kupatiwa mikopo kwa wingi bila ya matatizo kwakuwa watakuwa ni wanachama halali katika vikundi vya wakulima.

Ambapo takwimu zinaonesha kuwa kunavyama vya ushirika 718 vyenye wanachama 162,534 vyenye mtaji wa shilingi 31.7 bilion akiwasa kuwa idadi ya vyama ni ndogo ukilinganisha na idadi kubwa ya wananchi wanaoweza kujiunga na ushirika katika kanda.

Mwakipesile alisema ili kupata mitaji mingi ya mikopo mingi ni mhimu kujiunga kwa wanachama kwa wingi ili kuviimarisha vyama vilivyopo lengo kutotoa nafasi kwa wafanyabiashara walanguzi na makampuni kutonyanyasa wakulima na kuzuia Lombesa.
.
Aliviagiza vyama vya ushirika kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima ili kuweza kujiunga kwa wingi na kuwaelimisha athari ya kuuza mazao kabla ya kupitia vyama vya ushirika ili kuwaepuka walanguzi wa mazo wa mazo ya Kahawa, Kakao napareto kununuliwa kupitia vyama vya ushirika.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment