Photobucket

Wednesday, August 18, 2010

MBOLEA ZA RUZUKU ZIPELEKWE SEHEMU ZA KILIMO

Na Keneth Goliama,Mbeya.

WAKULIMA washauri serikali kuelekeza zaidi Mbolea za Ruzuku maeneo ambayo hujishughulisha kwa kilimo zaidi na sio kuweka maduka ya Mbolea Mjini kwani itapunguza uwizi wa mbolea za ruzuku katika usambazaji.

Wakulima hao pia wameomba serikali kuweza kuweka kiwango maalumu cha uuzaji wa Mbolea ili kuweza kuwanusuru wakulima wengi kununua mbolea katika msimu ujao wa kilimo.

Wakulima hao wakizungumza na Mwananchi walisema kunaumhimu wa serikali kuhakikisha inazuia matumizi mabovu ya mbolea za Ruzuku kwa msimu ujao wa kilimo ili kuruhusu wakulima kupata mbolea hiyo.
Anosisye Mwakyelyu alisema wakulima wamekuwa wakisumbuliwa katika kuhakikisha wanapataa mbolea za ruzuku licha ya Serikali kutoa Mbolea nyingi kwa wakulima hasa wa mikoa ya nyanda za juu kusini.

lnakuwa bado kunaukiritimba mkubwa katika ugawaji wa Mbolea na kuanzia kwa kupewa wasambazaji wa Mbolea hizo katika mkoa wa Mbeya kunakuwa na usumbufu kidogo katika upatikanaji wa Mbolea.

“Kwa kweli sisi sio watu wa Tanzania maana mbolea tunayopata inapatikana kwa tabu na ghari ukilinganisha na uzalishaji katika kila ekarii moja na kuwa hii sio azma ya serikali kuinua kilimo kwa wakulimabadala yake inatakiwa kupunguza gharama ya Mbolea na upatikana kuwa rahisi ili kuinua uchumi” Alisema Abeli Kamilo ambaye ni Mkulima .

Walisema kama watashindwa kupata suluhu bora ya uuzaji wa mbolea za ruzuku ili kuweza kuwafikia wananchi ni bora serikali ikapitia kasoro zilizojitokeza mwakaja kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.

Waliagiza kuwa serikali iache kutoa Mbolea za ruzuku nyingi halafu ikawaachia wachache ambao wanabaki kuwanyanyasa wakulima katika ukiritimba wao wa utoaji wa mbolea hizo.

Alisema suala la kuendeneza bodi maalumu ya kuhakikisha mbolea zinwafikia wakulima ipasvyo ipo mikononi mwa serikali na ndio wenye maamuzi.

Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakiesile alisema Serikali mwaka huu imepanga kuongeza kwa asilimia 18% ya Mbolea za ruzuku ili kuhakikisha azma ya serikali ya kilimo inakuwa imeongza mbolea.

Na kuwashauri wa wakulima kuongeza kilimo zaidi ili kuhakikisha wazalisha kiwango kikubwa sana kutokana na hali ya mvua kuonyesha vizuri.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment