Na Keneth Goliama,Mbeya.
KUKITHIRI kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi Jijini Mbeya kwa shamili kutokana na wananchi kuridharau jeshi la Polisi kwa madai limeshindwa kuwadibiti ipasavyo vibaka wanaosababisha kukosekana kwa usalama kwa wananchi.
Baadhi ya wananchi Jijini hapa walisema jana kuwa wameamua kuwashughulikia wahalifu hao wenyewe ili kuhakikisha waharifu wanapungua kwa kiasi kikubwa haja jijini na sio kuwaachia wpolisi ambao mara nyingi wanawaancha huru.
Wananchi ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema Jeshi la Polisi limekuwa likidhibiti matatizo makubwa na kusahau haya matatizo madogo ambayo yanakuwa kero kubwa kwa wananchi hasa hawa vibaka ndio maana Upigaji nondo umeanza kuzuka kwa kiwango kikubwa hapa jijini.
Maauaji ya Raia kupitia kwa wananchi wenye hasira kali yamekuwa yakishamili sana jijini hapa bila ya Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi chanzo cha wananchi kujichukulia sheria Mkononi.
“Juzi mpaka leo zaidi ya watu watatu wamekutwa mamekufa kwa kupigwa na wananchi kwa madai ni majambazi sugu huku sio kuchoshwa nao bali ni kutokana hata ukimwacha aktika kitua cha Polisi utakuta yupo mitaani na kujitapa hakuna mtu anayeniweza” alisema aliyetambulika bonifas.
Walisema kuna umhimu mkubwa wa Jeshi la polisi mkoani hapa kuhakikisha linashirikiana na Polisi ili kuhakikisha linakabiriana na waharifu ili kuhakikisha wananchi hawajichukulii sheria Mkonono.
Hata hiyo Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Advocate Nyombi alisema licha ya kuwa Jeshi la Polisi linakabiliwa na uhaba wa askari lakini limeweza kuhakikisha usalama unapatikana.
Nyombi aliwasii wananchi kuacha kuchukua sheria mkononi kwa madai hasira kali na badalla yake kuwafikisha katika vyombo husika ili sheria iweze kufanya kazi yake na kuwa wananchi watakao kamatwa kujichukulia sheria Mkononi kwa sababu ya hasira atafikishwa kaitika vyombo ya sheria kujibu.
Mwisho.
.
No comments:
Post a Comment