Photobucket

Wednesday, May 12, 2010

UK YATAPATA WAZIRI MPYA


Kiongozi wa chama cha Conservative, David Cameron, ndiye Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya Gordon Brown kujiuzulu Jumanne jioni.

BBC
WAKATI macho ya Dunia nzima yakitupia Nchi ya Uingereza kuangalia uchaguzi mkuu Bw Cameron, mwenye umri wa miaka 43, aliingia katiak makazi rasmi ya Uwaziri Mkuu wa Uingereza, 10 Downing Street, baada ya kuzuru Buckingham Palace, makazi ya Malikia wa Uingereza kwenda kupokea rasmi pendekezo la kumtaka aunde serikali mpya.

Alisema anakusudia kuunda "mseto kamili" na chama cha Liberal Democrats kuunda serikali imara na yenye utulivu".

Chama chake ndicho kilipata idadi kubwa zaidi ya viti bungeni katika uchaguzi uliofanyika juma lililopita, ingawa hakikupata uwingi unaotakiwa kuunda serikali bila kushirikiana na vyama vingine.

No comments:

Post a Comment