Namwandishi wetu.
WANAFUNZI wa chuo Kikuu cha Tumaini Daresalaam wapo tayari kukosa masomo kutokana na kushindwa kulipa ongezeko la ada ambalo limeanza kuwasumbua wengin wao na wegine kukosa matokeo kutokana na kushindwa kulipa ada.
Hayo yalieleezwa na na baadhi ya wanafunzi ambao wanasoma chuoni hapo na kukiasa chuo kuchukua juhudi za ziada kuhakikisha wanafunzi wote wanapata masomo licha ya ongezeko la ada kuwasubua baadhi yao.
Walisema licha ya chuo kutia jeuri na wazazi ambao ni washauri katika chuo hicho kukaa kimya kunaweza kukasababisha chuo hicho kukosa wanafuzi kutokana na ada kuwa kubwa.
Awali walisema baadhi yan wanafunzi wamekuwa wakivumilia ongezeko la ada lakini kadri ya miaka ikienda wamekuwa wakishindwa kujilipia kutokana na maisha ya kifedha kubadilika.
Wakigoma kutaja majina yao walisema ukweli kuwa ada ni kubwa haipingiki lakini cha kushangaza huduma zinazo tolewa katika chuo hicho ni kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na ada inayotozwa.
Walimuagiza mkuu wa chuo hicho Alex Malasusa kukaa na washauri wake kuhakikisha wanaangalia uwezekano wa kupunguza ada licha ya kugoma kupunguza ada .
Walisema kuwa Mkuu huyo haipingiki kuwa amesoma bure na kama anania ya kuendeleza elimu ya Tanzania hana budi kuwapunguzia ada wanafunzi ili waweze kupata elimu wengi na sio kama ilivyo sasa ambapo elimu ya Vyuo vya Tumaini inatolewa kwa ubaguzi wa kiuchumi.
Hata hivyo mwandish wa habari hii alipowasiliana wahusika wa chuo hicho hakuweza kufanikiwa lakini kwa taarifa zilizopatikana zinasema chuo hakipo tayari kushusha ada na kuwa atakayeshindwa aache chuo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment