Photobucket

Wednesday, May 12, 2010

SERIKALI YATAKIWA KUTOSUBIRI UCHAGUZI KUTATUA MATATIZO

Na Michael Mbughi,
ILEJE, MBEYA- TANZANIA
WAKAZI wa kijiji cha Mbebe wilayani Ileje wameiomba Serikali kutokusubiri uchaguzi kushughulikia matatizo ya wananchi bali kutekeleza malalamiko yao wakati wote.

Wakizungumza na JAIZMELA mwishoni mwa wiki wakazi hao walisema kijiji hicho kinakumbwa na tatizo la uhaba wa maji kuanzia mwezi ya Augast hadi pale mvua inapoanza kunyesha, lakini walisema kuwa licha ya kuchanga pesa toka miaka mitatu iliyopita hakuna kinachofanyika.

Eliakimu shimwela mwanakijiji wa mbebe alisema kuwa kila mwanakijiji alikuwa akichanga shilingi 2000 kwa ajili ya kuvuta maji kutoka kisima cha maji kilichopo eneo la Ipanga ili yafike kijijini hapo lakini pesa hizo hawaoni zinakokwenda maana hakuna maji hadi leo.

Kwa upande wake Godfry Minga ambaye naye ni mwanakijiji alisema kuwa serikali inaanza kufanya mipango ya utekelezaji inapoona uchaguzi ukikaribia lakini uchaguzi ukiwa mbali hatuwaoni viongozi wa kutembelea wanachi vijijini kama mbebe.

Minga alisema kuwa kwa sasa kila mwanakijiji anachanga shilingi 6000 kwa ajili ya maji na kudai kuwa leo hii kwa kuwa uchaguzi unakalibia ndiyo maana tumeona viongozi wa serilakali wameanza kuchora chora maeneo mbali mbali ya kupitisha maji lakini akadai kuwa endapo uchaguzi ukipita yawezekana utekelezaji huo ukaishia kwenye michoro hiyo.

Naye mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Nyasi alisema kuwa kwa sasa wanawake wanawakati mgumu kutokana na kuwepo kwa mauwaji ya watoto wadogo walio na umri chini ya miaka mitano.

Alisema kuwa kitendo cha watoto kuuawa mkoani humo kitawafanya akina mama wengi kutembea na watoto hao umbali mrefu huku wakitafuta maji kwa kuhofia kuwaaacha majumbani ambako alisema kwa sasa wanasakwa kama si binadamu.

Aliongeza kuwa wazazi walio na watoto wawili wadogo watakuwa na wakati mgumu kulazimika kuwabeba watoto wote wawili maana maji yanapatikana sehemu mbali nakudai kuwa aidha wengine watalazimishwa kuwasimamisha watoto wao shule ili wawalinde watoto kitu ambacho alisema nikibaya sana .

Afisa mtendaji wa kijiji hicho Robson Panja alikili kuwepo uhaba wa maji kijijini hapo na kudai kuwa jitihada za kutatua tatizo hilo zinafanywa na serikali ndiyo maana wakaona ni vyema wananchi waongeze kiwango cha kuchangia kufikia shilingi 6000 kuliko kile cha 2000 walichokuwa wakichanga ambacho alisema kisingeweza kusaidia kuvuta maji kutoka Ipanga.

Afisa mtendaji wa kata ya Mbebe Aina Kainga alisema kuwa wakazi wengi wa kijiji hicho wanashindwa kufanya mambo ya maendeleo ya kujiinua kiuchumi kutokana na kuhangaikia maji muda mwingi.

Aina aliongeza kuwa wanachi hao badara ya kujihusisha na mambo yamaendeleo kama biashara au mambo mengine yanayoweza kuwaongezea kipato, wanaishia kutafuta maji ambayo yanapatikana kwa umbali mrefu.

Aidha alisema serikali inatarajia kuanzisha mradi wa wa maji ambao alidai kuwa utawapunguzia wananchi hao kelo iliyopo ya maji ambayo alisema watavuta maji kutoka Ipanga hadi Mbebe nakudai kuwa kata hiyo iavijiji vine ambavyo alivitaja kuwa ni mbebe, Nashinji, Mtima na Mapagolo ila kijiji cha Mbebe ndicho kitapewa maji kwa kuwa ndicho kinauhaba zaidi kuliko vingine.

No comments:

Post a Comment