Na Keneth Goliama, Mbeya
WANANCHI wameshauriwa kutumia misaada wapatayo na wafadhili mbalimbali kuhakikisha zinatumika mahali zilipoelekezwa ili kuleta maendeleo zaidi.
Rai hiyo ilitolewa na Barnabas Mpozi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya vijini na ambaye ni Diwani wa Kata ya itewe wakati alipokuwa akiongea na viongozi wa kata zake kuhakikisha wanatumika katika maendeleo.
Mponzi alieleza kuwa jamii nyingi zimekuwa zikifuja misaada ambayo inatolewa na baadhi ya mashirika na makampuni katika ujenzi wa maendeleo .
Alisema kuwa umefika wakati kwa viongozi kuwa makini ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kile kinachoonekana kuhakikisha jamii inafurahishwa na wafadhili wanafurahishwa pia.
Mponzi alisisitiza kuwa kata zake zimekuwa zikipokea misaada mingi lakini maendeleo yamaekuwa yakipatikana kwa kiasi kidogo na hivyo wakati umefika kwa viongozi kuwa makini.
Alisisitiza kuwa shule zote zilizopewa misaada ikiwamo shule ya Msingi Mkapa katika kata yake zinatumiwa ipasavyo kuhakikisha zinafanikisha malengo ya serikari.
“Najua viongozi mna hamu ya kijiji chenu kupata maendeleo, wizi wa vifaa vilivyotolewa na waungwana wetu haufai kabisa nibora lawama lakini maendeleo yakapatikana katika kata yangu”. Alisema Mpozi.
Aliongeza kuwa kuanzia sasa atakakikisha anafuatilia misaada na maendeleo yote katika kata yake kujua maendeleo .
Alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia misaada kama njia ya kuneemeka lakini ole wao nitakao wakamata kuvuja fedha na mali za maendeleo yah pa kijjijini nitahakikisha tunawachukulia hatua kali za kishelia.
“Nawaombeni viongozi kufuatilia maendeleo ya jamii ili kuleta ufanisi katika jamii yetu na tukiwa waadilifu tutaweza kuleta maendeleo na kuwaondoa viongozi wachafu”a Alisema Mponzi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment