Na Keneth Goliama, Mbeya
ASKARI wa barabarani (Jina tunalo) juzi alitembeza kichapo kwa kondakta wa basi aina ya coaster yenye namba ya usajiri T208 AVJ linalofanya safari zake Mbeya na Tunduma ambaye alitambulika kwa jina moja kuwa ni Joel baada ya dereva wa gali hilo kukiuka sheria za barabarani za kutokuvaa sale alipokua akiendesha gali hilo.
Tukio hilo lilitokea wiki hii majira ya saa sita mchana katika eneo la Tazara nje kidogo na jiji la Mbeya mkoani hapa ambapo kondakta wa basi hilo aliamriwa na askari aliyejulikana kwa(jina la Limehifadhiwa) ambaye ndiye alikuwa mkuu wa zamu kwa siku hiyo ili akalipe faini ya dereva wake kwa askari mwingine aliyekuwa akishika kitabu cha risiti kwa kosa la kutovaa sale.
Lakini kondakta huyo alipoona kuwa aliyebaini makosa amebanwa na ukaguzi wa magari mengine ndipo akaamua kubadilisha kauli na kumwambia kuwa wameambiwa kwake ili alikaguwe gari lao wakati huo huo dereva akiwa ameshavaa sale yake aliyoipachika mbele ya usukani kwake.
Askari huyo alipoona kwamba gali halina makosa ndipo alipomruhusu dereva wa gari aondowe gali ambalo hata hivyo lilisimamishwa tena na mkuu wa zamu Maggie ambaye alitaka kuhakikisha kama kondakta amelipa faini aliyowaeleza kuilipa kwa Savera.
Askari alipobaini kwamba kondakta hajalipa faini ndipo alipoanza kumfokea askari mwenzake mbele ya kadamnasi kwa kosa la kutokuwalipisha faini bila kujua kwamba kauli yake ilipindishwa na kondakta alipokwenda kwa askari mwingine na kumwambia awalipishe faini kwa kosa lakutovaa sale.
Kitendo hicho kilimkera askari huyo baada ya kondakta kukubari makosa yakwamba kadanganya maelezo na kuona njia pekee ya kumuadabisha ni kumuwasha makofi mbele ya abiria waliokuwemo ndani ya gari na kuanza kumcharukia kwa matusi ili kuwa fundisho kwa waongo.
Kitendo cha askari huyo kutembeza kichapo mbele ya abiria kiliamsha hasira kwa baadhi wa abiria waliokuwemo kwenye gari lile na kuanza kumtupia maneno makali askari huyo na kusema anakiuka sheria za barabarani.
Abiria hao walisema haifurahishwi kuona Askari anachukua sheria mkononi na kuwa kwa nini asimchukulie hatua ya kwenda kumpeleka polisi na kumpa adhabu kali kuliko kumchapa vibao.
“Unabahati umemuona konda mwenyewe ni mpole tena mjinga wangekuwa wengine ungekiona chamoto kwa tabia yako yakumpiga”alisikika abiria mmoja ambaye jina halikuweza kupatikana.
“Kumbe siku hizi mmepata ujasiri kiasi cha kuwapiga makonda wakiwa wamepatikana na makosa madogo kama hayo? Ila mwisho mtaupata endelea na hiyo tabia au kwa kuwa mnatumia uaskari kwa kuwatishia wananchi! lakini mwisho mtaupata tu” alisikika abiria mwingine aliyejulikana kwa jina moja tu la Ambakisye .
Alipoulizwa na waandishi kwanini aliamua kuchukuwa sheria mkononi ya kumuadabisha kondakta kwa kumpiga makofi Askari huyo alisema “huwa mala nyingi hawa makondakta wanatabia ya kutuzarau sisi maaskari wa kike na ndiyo maana aliweza kunidanganya kwa kusema kuwa ameambiwa na mkuu wangu nilikaguwe gali kumbe alikuwa ameshakaguliwa wakati alitakiwa aniambie nimlipishe faini na ndiyo maana nikaamua kumpiga makofi”.
Askari huyo aliongeza kuwa wala hana makosa kwa kufanya kitendo kama kile na ndiyo maana aliamua kuwafuata wandishi wa habari walioshuhudia kitendo kile kwa kuwa ni jambo la kawaida kwa askari kuchukua sheria
“Hata hivyo hakuna sheria inayomkataza mwanamke kumpiga mwanaume eti kwa kuwa ni jinsia ya kike, isipokuwa ni kuheshimiana tu na ndiyo maana yule konda aliponivunjia heshima nikachukuwa hatua ya kumuwasha makofi, pili alitaka kunigombanisha baina yangu na mkubwa wangu kikazi lile ni kosa kubwa kwamgu” alisema Savera.
Hata hivyo dereva na kondakta baada ya kulipishwa faini waliendelea na safari yao kuelekea Tunduma huku abiria waliokuwemo kwenye gali wakiendelea kumtuhumu Askari kuwa amekiuka maadiri ya uaskali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment