Photobucket

Friday, April 9, 2010

Mkuu wa Mkoa John Mwakipesile Akifungua kituo cha Afya cha Marie Stopes kilichopo Mama John Mbeya



Na Keneth Goliama,Mbeya.
VIJIJI 98 vya mkoa wa Mbeya kupata huduma za bure za uzazi wa mpango na afya kutokana na ugumu wa kufikika kwa vijiji hivyo, vilivyoko mbali na hospitali kwa ajili ya kupata huduma ya afya.
Hayo yalielezwa na Asha Pamui Meneja wa kanda ya Pwani na kusini mwa Tanzania Marie Stopes katika ufunguzi wa kituo cha kutolea huduma ya afya mkoani hapa jana.
Pamui alieleza kuwa lengo la kuanzisha huduma hii ni kusaidia mpangom mzima wa huduma ya afya kufikia kila sehemu na kuhakikisha watu wanapata huduma bora.
Alieleza kuwa wananchi watapewa huduma ya afya bure kila kijiji ambacho kitanufaika na huduma hiyo na kuwa ni baadhi ya halmashauri zitakazofadika na mradi huo wa mkoba.
Pamui alizitaja wilaya zitakazo nufaika na huduma hiyo kuwa ni vijiji vilivyopo katika wilaya za Chunya,Rungwe, Mbeya vijijini,Ileje,Kyela ambazo huduma ya kuanza kuhudumia kuwa imeshakamilika.
“Napenda kutoa shukrani kwa viongozi wa wilaya kwa kukubali ubia wa huu wa kutoa huduma ya afya has kwa kuchangiwa dawa na vifaa pamoja na sehemu ya kutolea huduma katika zahanati za serikali” alisema Pamui.
Aliongeza kuwa serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kuhakikisha huduma inapatikana kila sehemu kwa kushirikiana na Marie Stopes kuhakikisha huduma inapatikana hapa nchini.
Alisema kuwa huduma za mkoba vijijini hutolewa kwa kufadhiliwa na na Marie Stopes International kupitia mradi uitwao SCALE UP ma mashirika mengine kwa kuiwezesha Mbeya kuingia katika mradi wa uzazi wa mpango hapa nchini.
Pamui alisema kuwa zaidi ya vituo 14 hapa nchini vinafanya kazi kuhakikisha huduma inapatikana na huduma hiyo ita husisha afya ya ukimwi na afya za akina mama za kufunga kizazi na kupimwa virusi vya ukimwi na kuchangia huduma za kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Watoto waliopata chanjo ni 36,773 na waliopima virusi vya ukimwi kuwa ni 37,953 pamoja na mgonjwa ya zinaa walipatikana wateja 49,004 ambao wamepata huduma za afya katika kituo cha Marie Stopes kwa mwaka 2009.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment