Na Keneth Goliama.
WAFANYABIASHA wa mazao ya chakula wailalamikia halimashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kuwatoza ushuru mkubwa huku wafanyabiashara wengine wakitozwa kiwango cha chini
Wafanyabiashara hao walisema umekuwa ni mchezo hapa wilayani kupandisha ushuru kiholela bila kuwashirikisha wadau husika nahivyo kufanya baadhi yao kulipa fedha ndogo za ushuru huku wengine wakilipa kiasi kikubwa.
Wakizungumza na Mwananchi katika soko la Mbalizi wilayani hapa walisema kikukweli hakuna bei maalumu ambayo wanaitambuka kutokana kuwa yapata miezi mitatu tu ushuru ulikuwa ni shilingi 400 lakini gafla umepanda kiasi kwambwa tunashindwa kufanya biashara za mazao hapa mkoani.
Wafanyabiashara hao walisema wameandika malalamiko yao katika ofisi husika lakini cha ajabu hakuna chochote kilichojibiwa zaidi ya watoza ushuru hao kuongeza kasi ya kuwasumbua wananchi ambao wanafanya biashara za mazao katika soko hilo.
“Kwa kweli hakuna ushuru uliopitishwa halali na vikao vya Halimashauri ili kuweza kusainiwa na Waziri mkuu ili kuweza kutumika katika kuwalipisha ushuru huo cha ajabu wamepandisha kutoka mia tano hadi shilingi1000 ambapo wafanyabiashata wadogo hatuwezi kumudu ushuru huo.” Alisema Godfrey ambaye ni mfanya biashara.
WAlisema kuwa uhakika wanao kuwa hakuna kitu chochote kilichopitishwa na waziri kwa ajili ya matumizi ya shilingi elfu moja kama ushuru kwa gunia cha ajabu wameamua kutumia ili kuweza kuwateas wananchi na wafanyabiashara katika mkoa huu.
WAfanyabiashara hao walisema nia ajabu kumsingizia waziri mkuu ili wo waogope kulipa na kuagiza kuwa kitendo hicho ni kwenda kinyume na sheria na kuwa hawapo tayari kufanya biashara na ushuru wa aina hiyo.
Walisema serikali imewapangia ushuru huo ambao ki ukweli kwa mfanya biashara hawezi kumudu gharama ya ushuru huo ambao ni zaidi ya nusu ya ushuru wa awali.
Mwanachi ilipo wasiliana na Msimamizi wa ushuru katika soko hilo alisema kuwa yeye sio msemaji wa halimashauri lakini ameamua kutoza ushuru wa shilingi mia saba kutokana na amri ya viongozi wake kumpa jukumu hilo.
Aliongeza kuwa ushuru huo umepanda kutokana na maamuzi ya halimashauri ya wilaya kuongeza ushuru kutokana na mahitaji na kuwa kuwatoza kiasi hicho cha mia saba kinatokana na na kuwa wafanyabiashara wengi kugomea shilingi elfu moja.
Hata hivyo wafanyabiashara wangi walipinga kaolin hiyo kuwa haina msingi kutokana kuwa upandishaji huo umekuwa wa gafla ukizingatia bajeti husika ni miezi michache tu kuonza.
Hata hivyo Mwekahazina wa Wilaya ya Mbeya Chamba Bigambo kwa niaba ya Mkurugezi wa Wilaya ya Mbeya alisema hafahamu kuwa kuna ushuru wa aina mbili na kuwa atalifanyia kazi.
Aliongeza kuwa wamepata malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara hao na kuwa vikao vya halmashauri vitaaza mda sio mrefu ili kuweza kuona malalamiko hayo ya wafanyabiashara yanafanyiwa ufumbuzi licha ya kuwa inapingwa na wengi kutokana na kutokuwa na elimu ya biashara.
Bigambo alisema wamekuwa wakipandisha kwa asilimia tano ya bei ya mazao na kuwa ushuru huo ni halali kwa mujibu wa sheria za halmashauri zilizopitishwa na waziri mkuu licha ya kuwa inapingwa na wengi kutokana na kutokuwa na elimu ya biasha.
No comments:
Post a Comment