Photobucket

Tuesday, April 20, 2010

MTKILA ACHEZA SINEMA NA POLISI

Kutoka Mwananchi

Waandishi Wetu
JANA ilikuwa kama sinema nyumbani kwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila wakati polisi walipomvamia kwa lengo la kumpekua na baadaye kumpeleka kituoni kwa mahojiano.

Polisi hao wa Kanda ya Dar es Salaam walivamia nyumba ya kiongozi huyo yenye na ghorofa mbili eneo la Mikocheni. Ilionekana kama Mtikila alitegemea ujio wao na hivyo hakutikisika wakati walipoingia na kuanza upekuzi.

Wakati wakiendelea na upekuzi uliochukua takribani saa tatu, Mtikila alikuwa akipokea simu mbalimbali kutoka kwa waandishi waliotaka kuthibitisha taarifa za kuvamiwa kwake na polisi na baadaye kufanya mkutano na waandishi huku upekuzi ukiendelea.

"Ndio polisi wako hapa wanapekuwa kwenye nyumba yangu kwa madai kuwa nimeandika waraka wa uchochezi... ukija utakuta wanaendelea kwa sababu nyumba hii ni kubwa; hawawezi kumaliza sasa hivi," alisema Mtikila kwa njia ya simu wakati Mwananchi ilipotaka kujua kama alikuwa akipekuliwa.

Na baada ya Mwananchi kufika nyumbani kwake, Mtikila alionekana hana wasiwasi wakati polisi wakiendelea kutafuta nakala za waraka huo. Waliikosa nakala na walipoamua kumchukua kuondoka naye, mchungaji huyo aliwaambia kuwa wasubiri kwa kuwa alitaka kuongea na waandishi na akakubaliwa.

“Kuna waraka ambao niliuandika na kuusambaza nchi nzima kwa waumini. Waraka huo unawataka Watanzania kujihadhari na Rais Kikwete...†Mtikila aliwaambia waandishi wa habari huku polisi hao waliovalia kiraia wakimsubiri.

Mtikila, ambaye alikiri mbele ya askari hao kuwa aliandika waraka huo lakini aliishiwa nakala zake hivyo wasingeweza kuzipata nyumbani kwake, alidai kuwa Rais Kikwete ni mdini na hivyo hafai kuchaguliwa tena.

Mwanasiasa huyo machachari, ambaye anakabiliwa na kesi nyingine ya kumkamshifu Rais Kikwete kuwa ni gaidi, alisema kuwa waraka huo sio siri tena kwa Watanzania kwa sababu alishausambaza sehemu mbalimbali nchini tangu mwaka jana.

Sakata hilo lilianza saa 2:15 asubuhi wakati polisi walipofika kwenye nyumba hiyo na kuizunguka, mithili ya askari wanaotaka kumkamata jambazi hatari. Baadaye waligonga mlango na kuingia ndani, kwa mujibu wa mke wa Mtikila , Georgia .

Georgia alilieleza gazeti hili kuwa askari hao walifika nyumbani hapo saa 1:00 asubuhi na hawakufunguliwa kwa kuwa hawakuwa na taarifa za ugeni wao asubuhi hiyo.
Alisema ilipofika saa 2:15 asubuhi mmoja wa majirani wao ambaye alifika nyumbani hapo kuwasalimu aliwaeleza kuwa nje ya nyumba hiyo kuna watu aliohisi kuwa ni askari ambao wanataka kuingia ndani.

Georgia, ambaye pia ni katibu mkuu wa DP, aliwaambia waandishi wa habari kuwa baada ya taarifa hizo walifungua mlango na askari hao wakaingia ndani na kumtaka Mtikila ambaye muda wote huo alikuwa bado amelala.

Alieleza kuwa askari hao walivalia kiraia na kueleza kuwa wamefuata waraka waliodai unasambazwa na Mtikila, ambaye aliwajibu kuwa umekwisha kwa kuwa ameshausambaza wote.
Majibu hayo ya Mtikila hayakuwaridha askari hao na ndipo walipoamua kuingia ndani na kufanya upekuzi na walipoukosa waliamua kuchukua kompyuta ya mezani aina ya HP na kuondoka nayo pamoja na mwenyekiti huyo wa DP.

Askari hao waliotumia gari aina ya Nissan yenye namba za usajili Z 801 BU walitoka na Mtikila aliyevalia suti nyeusi iliyonakshiwa madoa meupe na kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam .

Hata hivyo, Mtikila alisita kupanda gari la polisi na kuamua kuongea na waandishi wa habari ambao baadhi walifika nyumbani hapo baada ya kuitwa na Mtikila mwenyewe.

Waraka huo wenye kurasa 24 ambao Mwananchi imeona nakala yake, unamshambulia kiongozi huyo wa nchi ukimuhusisha na tuhuma mbalimbali, ambazo mchungaji huyo amekuwa akizitoa dhidi ya kiongozi huyo wa serikali ya awamu ya nne.

Baadaye mchana, kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa Mtikila amekamatwa kwa makosa ya jinai na habari zilizopatikana jioni zilieleza kuwa kiongozi huyo wa DP ameachiwa na anatakiwa aripoti kituoni leo.

Kova alieleza kuwa Mtikila atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Alisema hawezi kuendelea kuzungumzia suala la Mtikila mpaka atakapopata taarifa za kiupelelezi kutoka kwa vijana wake kwani bado upelelezi unaendelea.
“Ninavyozungumza hivi sasa, leo (jana) vijana wanafanya kazi ya upelelezi kwake Mikocheni kwa kufanya upekuzi na baadaye atafikishwa mahakamani,†alisisitiza Kamanda Kova.

Naye mwanaharakati wa haki binadamu, Julius Miselya amesema anashangazwa na kitendo cha polisi kumkamata Mtikila kwa makosa ya uchochezi na kumuacha Sheikh Yahya Hussein ambaye alitangaza kuwa atakayepambana na Rais Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao, atakufa.
Alisema ameusoma waraka huo na kuusambaza na hajaona sehemu yeyote inayomkashifu mtu

No comments:

Post a Comment