Photobucket

Friday, April 9, 2010

SHILINGI MILIONI 411 KUINUA ELIMU MBEYA

Keneth Goliama,Mbeya.

SHILINGI 411 milioni zatengwa kwa ajili ya elimu kwa mwaka 2010/2011 ambazo zitatumika kujenga nyumba za walimu, vyoo pamoja na madarasa ili kuhakikisha inakabiriana na upungufu katika sekta ya elimu katika halimashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Hayo yalisemwa jana na MKurugenzi wa mtendaji wa wilaya ya Mbeya Juliana Malange katika kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) kilichokuwa kikipitia makisio ya mapato na matumizi ya halmshauri ya Wilaya ya Mbeya ya mwaka 2010/2011.
Alieleza kuwa katika makisio hayo Wilaya ya mbeya inatarajiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha katika ujenzi wa nyumba za walimu katika shule za msingi ili kuhakikisha walimu wanapata hifadhi.

Malange alisema kuwa kuna baadhi ya shule zimekuwa zikikosa walimu kutokana hakuna nyumba ambayo inaweza kuhifadhi mwanilimu na hivyo kufanya uboreshaji wa elimu kuwa mgumu.

Aliongeza kuwa suala la kuweka kiasi kikubwa ni kuhakikisha malengo ya Wilaya ya kuinua kiwango cha elimu kuna panda na na kuvuka malengo ili kuwa na elimu bora zaidi

Malange aliongeza kuwasekta hii imetengewa kisai hichi ili kuhakikisha fedha hizo zinatumikas kujengea nyumba za walimu katika elimu ya msingi na katika sekondari zitatumika kujengea madarasa na pamoja na vyoo kuhakikisha matatizo madogo madogo yanakamilika .

Alieleza kuwa halimashauri ya wilaya Mbeya imefikia malengo asilimia 100% ya wanafunzi wake wengi wamechukuliwa kwenda sekondari hii ni kutokana na kuwa makini kuhakikisha ujenzi wa shule unakamilika.

Ujenzi huo unatarajia kujenga nyumba 22 za walimukwenye shule za msingi utakao gharimu kiasi cha shilingi 156.2 milioni kuhakikisha uhaba wa nyumba za walimu zinapunguzwa ambazo shule zitafaidika mijawapo ni Itambalila,Kawetere Pashungu,Lwanjiro,Mbonile,Masewe Insoso,Shuwa,Nsenga na zinginezo.

Alieleza pia kuwa katika elimu ya sekondari licha ya kuwa halmashauri kwa kiasi kikubwa imejitahidi lakini kuta kuwa na ujenzi wa madarasa saba na ujenzi wanyumba za walimu nne pamoja na ujenzi wa vyoo vitano jumla vyenye thamani ya shilingi 155.4 milioni katika sekondari.

Alieleza kuwa malengo hayo yanatokana na kuwa na vyanzo mbalimbali ya mapato katika halmashauri ya wilaya kwa kuhakikisha wanakusanya kwa makini ka kufanikisha malengo ya mwaka ujao wa feha katika halmashauri.

Malange aliwaasa watendaji wa watumishi kuhakikisha wanatumia vizuri fedha zitakazotumika kujenga maendeleo ya elimu katika halimashuri na kuwa hatamvumilia mtumishi yeyote atakaye fanya uzembe.

“Tutakapokuwa makini katika ujenzi wa elimu tutakuwa tunajenga watoto wetu waende shule na sio tuwaache wakiwa wanahangaika wakati mapato yetu yanaonyesha kufanikiwa kwa ujenzi wa shule. “alisema

Malange alieleza sekondari ilizopewa kipaumbele kuwa ni Iwalanje ambayo itakuwa ni moja ya shule zitakzopokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita kwa mwaka huu na baadhi ya sekondari kuwa ni Malawe ,Shibolya Mwaselela na Songwe katikan ujenzi.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment