MBEYA, TANZANIA
Vitendo vya uvutaji bangi, ufisadi, utoaji mimba na uuaji wa watoto, chanzo chake ni malezi mabaya ya familia
Hayo yamedhihirika mkoani Mbeya ambapo watoto zaidi ya 2000 wa Shirika la Kipapa Jimbo la Katoliki Mbeya kufanya Maadhimisho ya Tisa ya Familia Takatifu ya Kanisa hilo Desemba 27, mwaka huu.
Watoto hao waliovaolia mavazi ya rangi ya manjano na nyeupe walianza maandamano saa 4:00 asubuhi kutoka Kanisa dogo la Parokia ya Mwanjelwa kwenda Kanisa la Hija la Bikira Maria wa Fatima Jimbo Katoliki mkoani hapa ambako ibada ilifanyika.
Ibada ya siku hiyo iliongozwa na Mhashamu Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo Katoliki Mbeya mahususi kabisa kwa ajili ya watoto hao.
Akiongoza Ibada Mhashamu Askofu alisema ukiiona jamii nzuri na yenye maadili uje fika kwamba familia iliwekwa kipaumbele.
Akimnukuu Papa John Paul II alisema familia ilivyo ndivyo na Taifa
Aliendelea kusema kuwa nchi ya Tanzania ina wasomi wengi lakini na wamesahau walikotoka na hiyo ni dalili kuwa ufisadi hauwezi kuisha.
Akisititiza kuhusu hilo alisema ufisadi hutokea kwasababu ya Ubinafsi katika mioyo ya watu na ndio maana wasomi wengi wamekazana kujenga mijini na kusahau kwamba kuna siku watatamani kurudi walikotoka ambako ni vijijini.
Pia aliwapongeza wazazi kwa kuwalea watoto vizuri japo ya changamoto wanazokutana nazo kila siku.
Mhashamu Askofu alihitimisha ibada hiyo kwa kutoa mwito kwa wazazi kudumisha upendo katika familia na kumlingana Mungu na kusema kwamba kitendo cha Papa Benedict XVI kuvamiwa na msichana wakati akipanda madhabahuni mapema mwezi huu ni malezi mabaya ya familia aliyotoka msichana huyo.
Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kuongea na mwandaaji wa Maadhimisho Padre Innocent Sanga na kusema wamejipanga vizuri kwa sherehe nyingine mwakani maana za safari hii zimemtia moyo sana kwa wingi wa watoto tofauti na zilizopita tangu mwaka 2001.
Maadhimisho hayo yaliwaleta pamoja watoto kutoka Parokia za Tukuyu, Isanga, Inyara, na Mbeya Mjini mahususi kwa kuombea watoto na kudumisha upendo katika familia.
No comments:
Post a Comment