Na Keneth Goliama, Mbeya
WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoa wa Mbeya kikipata viongozi wapya wa nafasi ya Mwenyekiti na Katibu,wajumbe 14 wa wilaya ya chunya wamesusia kupiga kura huku wakimtoa nje mmoja wa mgombea wa nafasi ya umwenyekiti kwa madai kuwa kulikuwa na njama za makusudi za kumpitisha mgombea aliyeshinda.
Msimamizi wa uchaguzi kutoka makao makuu ya chama hicho Taifa Susana Kiwanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa wanawake wa chama hicho mkoa wa Morogoro alisema kuondolewa kwa baadhi ya wajumbe hao wa wilaya ya Chunya kunatokana na kubainika kuwa ni mamluki.
Hali hiyo ilitokea jana mkoani hapa katika ukumbi wa ‘Cofee Garden’ ulioko karibu na uwanja wa mpira wa sokoine wakati chama hicho cha Chadema kikifanya uchaguzio wake wa pili baada ya ule wa awali ulifanyika Agosti mwaka jana kuvunjika kutokana na vurugu zilidaiwa kusababishwa na shutuma za kuchomekewa mamluki.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi huyo Susana Kiwanga,alisema hatarajii wala kuamini kuwa uchagu huo haukuzingatia haki kwa kuwa taratibu zote zilifuatwa na kasoro zilizojitokeza ni ndogo jambo ambalo lisingesababisha uchaguzi kuahirishwa tena.
Aliwataja walioshinda nafasi ya uenyekiti kuwa ni wakili wa kujitegemea mkoani hapa Sambwee Shitambala aliyepata kura 34,huku mpinzani wake aliyeondolewa na wajumbe wa chunya ikiwa zimebaki dakika chache kuingia kujieleza alipata kura 6.
Nafasi ya Katibu mpya wa mkoa ilichukuliwa na Eddo Makata aliyepata kura 31 na kumshinda mwenzake wa nafasi hiyo Ipyana Seme aliyeambulia kura 9 tu.Wajumbe ambao walienguliwa ni kutoka katika jimbo la Mbozi Lupa na Chunya Mbeya mjini .
Wakizungumza na Mwananchi baada ya kutoka nje ya ukumbi huo wa uchaguzi wajumbe waliokataliwa kwa madai kuwa mamluki walisema wameshangazwa na kitendo hicho kwa kuwa wao ni wajumbe halali ambao katika uchaguzi mkuu wa taifa waliingia kama wajumbe halali.
“Demokrasia muda mwingine ni kama dhahama kwa watu wengine,inashangaza katika uchaguzi wa taifa tuliingia lakini leo tunazuiwa ” alilamika mmoja wa wajumbe hao kutoka jimbo la Lupa wiyani Chunya.
George Mtasha Mwenyekiti aliyekuwa akitetea kiti hicho alipotakiwa kueleza sababu za yeye kukubali shinikizo la wajumbe hao 14 na kususia zoezi hili alisema alifanya hivyo ili kulinda maslahi ya chama.
“Nisingeweza kuwakatali watu wangu ,kumbuka hawa ni wanachama wa wenye ushawishi mkubwa na hapa tayari wanatishia kurudisha kadi za chama unafikiri itakuwaje” alihojo Mtasha.
Hata hivyo alisema huenda jitihada za msimamizi wa kutaka kuwapitisha watu wanaowata linatokana na ngazi ya taifa huku akionekana dhahiri kurejea makundi yale yaliyojitokeza katika uchaguzi mkuu wa taifa ulifanyika mwaka jana na kuzua mtafaruku mkubwa.
Aidha, jeshi la Polisi mkoani hapa liliamua kuingilia kati ili kutuliza hali ya mambo baada ya mzozo ulioibuka ukumbuni hapo kwa wajumbe waliotimuliwa kutishia kuleta vurugu endapo mgombea waliyehisi kuonewa kama angeshinikizwa kuingia katika chumba cha kupigiwa kura.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment