Photobucket

Thursday, September 8, 2011

MAOFISA WALIOFANYA MSAKO KWA WASIO NA VYOO WAKAMATWE MARA MOJA



Na leo Tanzania
 MKUU wa mkoa wa Mbeya Bwana John Mwakipesile (pichani) amewaagiza viongozi wa  wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe kuwachukulia hatua za kisheria watumishi waliokwenda kuwanyanyasa wananchi katika kata Kisiba kwa madai ya kufanya msako wa wakazi wasiokuwa na vyoo.

 Mkuu huyo wa  mkoa alisema  watumishi hao ambao ni maafisa wa afya wakishirikiana na baadhi ya watendaji katika kata hiyo waliendesha zoezi hilo mapema wiki hii ambapo amelalamikia taratibu walizokuwa wakizitumia dhidi ya  wasio na vyoo haikuwa ya haki kutokana na  kunyang’anya mali zao.

Akizungumza wakati wa baraza maalumu la madiwani wilayani Rungwe kilicholenga kujadili taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG alisema ni kosa kabisa kufanya msako huku mkihisisha vitu ambayo havikuwa katika ajenda.

Bwana Mwakipesile amesema maofisa hao waliwatoza fidia za aina tofauti wananchi hao wakiwemo wazee wasiojiweza pasipo kuwapa stakabadhi hali inayodhihirisha kuwa zoezi hilo lililenga maslahi binafsi.

Ametoa siku hadi jumatatu ya wiki lijalo kupelekewa majina ya maofisa hao ofisini kwake ikiwa ni pamoja na hatua zilizochukuliwa dhidi yao.


No comments:

Post a Comment