Photobucket

Saturday, December 11, 2010

WAHADHILI NA WANFUNZI WATAKA MIAKA $( YA UHURU IKUMBUKWE KATIBA MPYA


a Keneth Goliama, Mbeya.

WAHADHILI na wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Mbeya wametaka miaka 49 ya uhuruku ikumbukwe katika kuanza kulenga na kufikiri katiba mpya ili kuweza kutoa haki sawa kwa wananchi pamoja na katiba kuendana na mifumo mizima ya utendaji wa sasa na unaoendelea.

Pia waliongeza kuwa miaka hiyo ikumbukwe katika kubadilisha vigezo vya ajira ili kuweza kuruhusu vijana wengi kuajiliwa kutokana na mfumo mzima wa utoaji wa ajira kupitwa na wakati.

Walisema vijana wengi wanakabiriwa na sifa za kuajiriwa hasa kigezo cha uzoefu ambacho mara nyingi huweka miaka mitano au kumi hivyo kufanya wanaoajiriwa kuwa wazee tu kutokana na kijana anyemaliza chuo kwa kiasi kuwa na miaka zaidi ya 26

Wakizungumza katika mdahalo miaka 49 ya uhuru Tanzania bara na inakoelekea walisema kuna umhimu mkubwa wa kupata katiba mpya ili kuweza kujua na kuimarisha demokrasia ya kweli.

Walisema nguvu ya mahitaji ya wakati ule ambapo katiba ilitengenezwa ni tofauti na sasa kuwa maendeleo ya nchi yanakwenda kinyume na katiba hiyo na kuasa kuwapuuzia wale wote wanaobeza fikra za katiba mpya

Alisema Tanzania ni tajiri kupindukia lakini nimasikini tena kupindua kia kutokana na katiba ya kuonyesha inakumbatia wageni kuliko wenyeji hasa kwenye rasilimali ya Taifa.

Mmmoja ya wanafunzi chuo cha Teofilo kisaji (teku) alisema katiba mpya ndio suruhu ya watanzania na kuwasihi viongozi kuacha kubeza malengo ya taifa maana kukata kubadilisha katiba ni kuruhusu maliasili za taifa kuendelea kufujwa ovyo bila kushughulikiwa na kuwasihii watanzania kuonyesha dhamila ya katiba mpya

Nao wanafunzi wa chuo cha mzumbe waliosimama kuchagia mjadala huo walisema anaekataa katiba mpya lazima aulizwe anasherekea nini miaka 49 ya uhuru wakati katiba inazidi kuweka viraka hadi aibu suluhu ya yote ni kuunda katiba mpaya.

Hata hivyo mhadhili wa chuo cha Teku chambanenge alisema wanosherekea miaka 49 wajiulize nini wameifanyia Tanzania na wanamalengo gani na kumtaka rais miaka hiyo kuchukua makali yake kwa kuwashughulikia mafisadi wote.

Alisema Taifa kubwa kama Tanzania linatakiwa kuheshimu mchango wa vijana na kuachana na fikra mbovu za kuwa vijana Taifa la kesho na sasa kuwatumia ipasavyo katika maendeleo ili kukuza uchumi na kisiasa.

Mgeni rasmi wa mdahalo huo alikuwa Profesa Tully kassimoto ambaye ni makamu mkuu wa chuo cha TeKU aliseama wanafunzi wanatakiwa kutumia elimu yao katika kufafanua, kuangalia vitu vinavyojitokeza siku hadi siku

Profesa Kassimoto alisema jukwaa hilo litumike katika kujitambua wako wapi wanaenda wapi na wametoka wapi ili kuweza kujua mchango wao katika miaka 49 ya uhuru.

Mdahalo huo wa miaka 49 ya uhuru Tanzania bara umelenga kutoa changamoto na mafanikia kwa serikali kiuchumi kisiasa kijamii na nafasi ya mwanamke katika mendeleo ya nchi kwa kushirikisha vyuo mbalimbali ikiwepo Chuo cha Uhasibu, Mzumbe, Teku

Mwisho

No comments:

Post a Comment