Na Keneth Goliama, Mbeya
ASKOFU wa Katoliki jimbo la Mbeya Evalisto Chengula ametoa kipaimala kwa wafungwa 20 wa Gereza la Ruanda lililopo jijini Mbeya baada ya kumaliza masomo yaliyokuwa yakiendeshwa na kanisa hilo magerezanikwa wafungwa wote.
Taarifa zilizotolewa na tume ya haki na amani jimboni mwishoni mwa wiki hii zilisema kuwa kanisa katoliki limeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo ya kiroho kwa wafungwa wote walioko katika magereza ya songwe, Ruanda, Kyela, Vyawa, na Ngwala ambapo wafungwa 20 tayari wameshapata kipaimala.
Ilisema kuwa lengo la kuendesha huduma ya kiroho ni kuhakikisha wafungwa wanajitambua kuhusu kosa walilolifanya na kukubari kujirudi na kujitayarisha kujumuika na jamii baada ya kumaliza vifungo vyao na kuwa raia wema.
Taarifa ilieleza kuwa wafungwa wanahimizwa kuwa na upendo wenyewe kwa wenyewe kwa kushirikiana na wafanyakazi wa magereza ili waishi kwa uadilifu na kumuogopa mungu kwani kujifunza makosa nio kujiimarisha katika kuishi na wananchi.
Chengula alisema katika kutekeleza huduma ya kiroho baadhi ya wafungwa wameshabatizwa na kuwa huduma hiyo itaendelea kuwaweka wafungwa katika kuonekana wamekosa hivyo kutubu ili kumrudia mungu na kuishi maisha ya kumpendeza mungu baada ya kutoka kifungoni.
Askofu Chengula alitoa wito kwa wafungwa wote na wafanyakazi wa magereza kuwa wapewe moyo wa uvumilivu na pia wafungwa baada ya kumaliza vifungo vyao ili waweze kurudi katika i kwenye jamii na kuendelea na maisha adilifu.
Askofu huyo aliomba jamii kutokuwanyanyapaa wafungwa ambao wamemaliza vifungo vyao bali wawasaidie katika kuwapa huduma ya kiroho akidai kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kumfanya mtu atambuwe makosa aliyoyafanya.
“Tukiwapenda ndugu na jamaa waliomaliza vifungo vyao katika magereza na kuwaona wamemrudia mungu kwa kutambua makosa waliyoyafanya wataishi maisha ya amani na upendo katika kuleta maendeleo ya jamii na kiroho.
Alisemawameona umhimu wa kuwapa elimu ya kiroho wafungwa wote katika mkoa wa Mbeya na kuwasihi makanisa mengine kufanya tendo hilo ya kuwaelimisha wafungwa kimwili na kiroho ili waweze kuishi kwa upendo watokapo gerezani
Huduma hii ya kiroho kwa wafungwa imekuja baada ya kutambua umhimu wa kuwapa mafunzo watu waliopo magerezani ambao hujiona kama wametengwa na jamii na kuwa kuwa karibu nao kutasaidia kujitambua makosana kukubali kujirudi kuwa waadilifu
MWISHO.
No comments:
Post a Comment