Photobucket

Friday, September 3, 2010

WANAFUNZI 1392 WAPEWA MIMBA

WANAFUNZI 1392 wa shule za Msingi na Sekondari mkoani Mbeya wameacha masomo yao kutokana na kushika mimba wakiwa shuleni katika kipindi cha 2006-2009 imebainika.

Akizungumza katika mahojiano maalum Afisa Elimu wa mkoa wa Mbeya Juma Kaponda alisema “takwimu hizo ni za kusikitisha kwani hakuna anayependa mtoto wake wa kumzaa aache masomo kwa sababu ya mimba”.


Aliongeza kuwa “katika kipindi hicho mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi zilikuwa 668 na wa sekondari zilikuwa 724 mimba katika shule za msingi zimepungua sana ukilinganisha na miaka ya nyuma na cha kushangaza zaidi ni kwamba mimba nyingi zisizo tarajiwa zipo katika shule za sekondari”.


Hata hivyo Kaponda alizitaja sababu za mimba katika shule za misingi kupungua na za sekondari kuongezeka kuwa ni umri mdogo wa watoto wanaoingia darasa la kwanza tofauti na miaka ya nyuma ambapo mtoto alikuwa akiingia darasa la kwanza akiwa na miaka zaidi ya 9.


“utaona kuwa katika shule za sekondari mimba zimeongezeka kutokana na shule hizo kuwa nyingi ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo zilikuwa chache pia wanafunzi kuwahi kuingia sekondari nako pia kumesababisha ongezeko hilo”.


Pia alisema kuwa wanfunzi wa kidato cha kwanza na cha pili mkoani hapo ndio wameonekana kuathiriwa zaidi na tatizo hilo la mimba wakati wa masomo na huenda umakini wa wazazi kutowalea vizuri wanapokuwa majumbani na kwa kufanya hivyo hata walimu watakaotoka katika kundi hilo nao watakuwa wabovu.


Kaponda alitoa wito kwa wanafunzi kujikinga na hali hiyo kwa kujiepusha na vishawishi vitakavyosababisha wao kujiingiza katika tama hatimaye kupata mimba, vilevile kwa walimu aliwataka wasimamie maadili yao kwani ni jambo la kushangaza mwalimu ambaye mwanafunzi anategemea kupata hekima na busara kutoka kwake anapokuta wapo katika uhusiano wa kimapenzi.

No comments:

Post a Comment