Photobucket

Wednesday, August 18, 2010

MBUNGE WA CCM AHAMIA CHADEMA NA KUTOA SHUTUMA KWENYE MCHAKATO WA MAONI

Na Keneth Goliama, Mbeya.

ZIMWI wagombea wa chama ca mapinduzi( CCM) walioshindwa kura zamaoni kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lazidi kuivuruga CCM Mbeya.

Aliyekuwa Mbunge wa CCM Paul Edward Mtwina jimbo la songwe ahamia CHADEMA na kutangaza nia ya kugombea ubunge ili kumvaa mpinzani wake Philipo Augustino Mlugo kwa madai ya kuendekeza rushwa nadi ya chama hicho.

Akikabidhiwa kadi na mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya Sambwee Shitambala katika makao makuu chama hicho alisema ameamua kuhamia chadema kwasababu wananchi wa songwe wanahitaji maendeleo na sio maneno.

Mtwina alisema kuhamia chama pinzani ni kuonyesha dhahili kuwa hakubaliani na maamuzi ya kura za maoni kutokana na wapinzani wake kumwaga wanafunzi kwenda kupiga kura ili kushinda.

Alisema CCM imekuwa ikiwatetea watu wasiojua kuongea na kutetea maslahi ya wananchi ili kuweza kuwaburuza wakati wa maamuzi ya maendeleo kwa wananchi na kukukumbatia Rushwa.

“Nimeamua kuhamia chadema kama maamuzi yangu binafsi kwakuwa wananchii wananihitaji kugombea kwa kuwa zamani nilikuwa nafanya kazi zangu na chma Mwenyekiti wa wazazi ccm jimbo la songwe na kaada wa TANU”.alisema mtwina.

Alisema chadema wanamisingi bora ambayo inafuata miiko ya Tanu na nichama kinachohitaji maendeleo ya wannanchi na sio kukumbatia ufisadi na rushwa.
Mtwina alisema hajutii kuwa mshindi wa pili kwa sababu fedha nyingi zilimwagwa na wanafunzi wengi walipelekwa kupiga kura ili kuweza kufanikisha ushindi wa mpinzani licha ya kupeleka malalamiko yake imekuwa ni kutetea ufisadi.

Aliongeza kuwa kuna matatizo mengi kwa wananchi wa jimbo la songwe ikiwa ni kukosa barabara ,maji ambayo wanatumia ya mtoni wakati wanavitu vingi vya kujivunia ikiwa madini kama ngwala mine ambayo yanachukuliwa na wezetu tu.

“Wananchi wananchi wachimbia guzo za umeme lakini serikali haija ona faida kwa wananchi ndio maana hakuna umeme kwani ni wilaya ya kwanza kuingiwa na wazungu kuibiwa mali zetu na si tupo kimya.” Alisema Mtwina.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa SAmbwee Shitambala alisema hii ni dalili tosha CCM kupoteza mwelekeo kwa kuwa CHADEMA inataka dola ya kuwaletea maendeleo wananchi na sio kuwanyang’anya maendeleo.

Aliongeza kuwa hakubaliani kabisa na kauli ya Katibu wa CCM kuwa kuhama CCM ni kushindwa kisiasa na kama dhambi ya mauti, bali ni kutaka kuleta mapinduzi na maendeleo bora kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment