Brandy Nelson, Mbeya
NI vita ya ushindani wa kibiashara ilikuwa imehamia barabarani baada ya malori mawili ya kampuni zinazopambana vikali katika biashara ya vinywaji laini, Pepsi na Coca-Cola kugongana na kusababisha vifo vya watu watano.
Magari hayo, Mitsubishi Fuso linalomilikiwa na kampuni ya SBC
inayotengeneza soda za jamii ya Pepsi, na Mercedes Benz linalomilikiwa na Coca-Cola yaligongana eneo la Mlima Senjere kwenye barabara ya Mbeya/Tunduma wakati gari moja likitaka kulipita lori lililokuwa limebeba bia.
Chriss Kashiririka, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema dereva wa Fuso, Benedict Sanga, 50, alikuwa akijaribu kulipita gari la Coca-Cola lililokuwa likiendeshwa na Henry Mbalah, 38, lakini ghafla akaliona lori lililobeba bia likipandisha mlima na hivyo kuamua kurudi kwenye njia yake na kujikuta akiligonga kwa nyuma Benz hilo.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Advocate Nyombi Waliokufa katika ajali hiyo ni pamoja na dereva wa gari ya Pepsi (SBC) Sanga ambaye ni mkazi wa Sae, afisa mauzo wa Pepsi, Martha Mushigati, 32, mkazi wa Forest, Enos Elia, 32, mkazi wa Iyunga na Samuel Thomas, 25 mkazi wa Nzovwe ambao walikuwa vibarua kwenye gari hilo la Pepsi.
Mwingine ni dereva wa kampuni ya SBC aliyekuwa ameacha gari yake katika mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi na kupanda gari hilo laPepsi, Albert Mbanga, 38, ambaye ni mkazi wa kitongoji cha Uyole jijini Mbeya.
Kamanda Nyombi amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2:00 usiku na kwamba miili ya waliofariki imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendo wa kasi wa gari hilo la SBC wakati akishuka kwenye mteremko huo na kushindwa kudhibiti breki zake.
Kamanda Nyombi alisema katika ajali ya pili iliyotokea jana saa 02:45 usiku eneo la Nzovwe jijini Mbeya, mpandabaiskeli aliyefahamika kwa jina moja la Nick alikufa papohapo baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Hiace iliyokuwa ikiendeshwa na Nicholous Masebo mkazi wa Nzovwe ambaye anashikiliwa na jeshi hil
No comments:
Post a Comment