Photobucket

Friday, September 3, 2010

WAKULIMA WAMLILIA SOKO KUUZWA KWA MKURUGEZI

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KIWILA WAKISHANGILIA KUONA WAADISHI WA HABARI

Na Keneth Goliama,Tukuyu.


ZAIDI ya Wakulima 600 wamlilia Rais Jakaya Kikwete katika soko la kiwira lililopo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya kutaka kupunguziwa ushuru ndani ya soko hilo pamoja na kuiondoa familia moja inayokusanya ushuru.
Wakulima hao pia wamemuomba Rais Kikwete kuingilia kati suala hilo la kutozwa ushuru mkubwa na kudai kuundwa bodi maalumu ya kukusanya mapato badala ya familia moja kufanya kazi ya kukusanya ushuru na hivyo kukandamiza wakulima kwa masilahi yao binafsi.


Wakulima hao waliotoka vijiji mbalimbali walikusanyika katika soko hili huku wengine wakilia baada ya kikundi cha mabausa kilicho wekwa na mkurugenzi wao kutumia nguvu kuwanyanganya bidhaa walizokuja kuziuza kwa madai hawajalipia ushuru.


Wakulima hao waliowahi kuzuia msafara wa la Rais oktoba waka 2008 kuomba kujengwa kwa soko la kiwira kutokana na baadhi ya wakazi wa sehemu hiyo kugongwa na gari na hivyo kusababisha kupoteza kwa maisha ya watu wengi
wamemtaka Rais kutaka kuwanusuru kutokana na manyanyaso yanayopatikana sokoni humo kuwa ni bora hata wakimbizi wanao ishi hapa nchini.


Wakizungumza na waandishi wa habari katika soko hilo la Kiwira wakulima hao walisema wanaomba Rais kuwasaidia kama alivyowaahidi kuwajengea soko na kufanikisha na hivyo wanamuomba msaada wake kwa kuwanusuru wakulima hao.


Walisema wamekuwa wakisumbuliwa sana kutokana na kupandishwa ushuru kutoka shilingi 100 hadi 300 kwa mkulima na hivyo kushindwa kumudu gharama hizo ambapo hata shambani wanakotoka wanalipa ushuru huo.
“kwa kweli sisi sio watu wa Tanzania maana ushuru tunaolipa ni nkubwa sana kwani nalipa shilingi mia tatu wakati kroba kimoja nauza shilingi elfu mbili , tukishindwa kulipia wanatupiga huku wakinyang`anya mboga zetu tukulipa Mboga hawaturudishii kweli ni haki jamani.” Alisema Abeli Kamilo ambaya ni Mkulima.



Wakulima hao walisema mkurugenzi amevunja bodi iliyokuwa ikikusanya ushuru na kuleta watu wasiojulikana ambao wanatumia mabavu kukusanya ushuru na kunyang`anya bidhaa za wakulima na kutupa mboga za wakulima hao .


Walisema kama watashindwa kupata suluhu ni bora soko likavunjwa halafu watu waendelee kufa pale barabarani kwa ni imekuwa kero kwa wakuli ambao hawana uwezo wa kulipia ushuru huo.


“Shida na kilio chetu kikubwa ni ushuru kwa soko hili maana umepanda gafla usione tumekusanyika hapa ni kutaka viongozi wajuu wajue tunavyo teseka maana haya ni maisha mabaya kwa kilia mtanzania ,ni bora Rais atusikie maana hii sio haki” alisema Betrice mwakusya muuza mifagio.


Wakulima hao walisema awali wakikabidhiwa soko hilo kuwa la kimataifa cha ajabu soko hilo la kimataifa limekabidhiwa kwa mtu mmoja aliyepewa jukumu la kukusanya mapato ambapo hakuna taarifa zozote zilizotumika kuleta mkusanyaji huyo.
Walisema wamekuwa wakimpa malalamiko kwa mkurugenzi wa wilaya ya Rungwe cha ajabu amekuwa mkali kama mbogo kwa kufokea na hivyo kumwogopa kutokana hataki kusikiliza matatizo yao.
Aidha wakulima hao walisema hawa wanaonunua mahindi vijijini wanakatwa ushuru lakini wakifika getini hapo wanakatwa ushuru na bado wakiingia ndani ya soko wanakatwa ushuru ni kweli ushuru gani huo walihoji wakulima hao.


“Tunasema hivi mwandishi iwapo kama vionogozi wetu hawatakuwa tayari kusikia kilio chetu kamwe hatuta kuwa tayari kuvumilia mateso hayo maana mkurugenzi anaenda kinyume na maagizo ya rais sisi ni watu timamu” walisema wakulima hao.


Waliagiza kuwa serikali iache kujenga masoko na kuwaachia wachache ambao wanabaki kuwanyanyasa wakulima na kuwa wanamuomba Rais na serikali yake kutupia macho soko hilo.


Naye Mkurugenzi wa Wilaya Rungwe Noel Mwahyenga alisema anachotaka ni kukusanya mapato kutokana na kuwa waliokuwa wakikusanya mapato walikuwa wanaletashilingi laki sita lakini kwa sasa wanaleta shilingi milioni 2.1 kila jumanne na kufanya makusanyo hayo kwa mwezi kuwa shilingi 8.4 .


Alisema suala la kuvunja bodi ya kwanza ipo mikononi mwake n a kuwa aliyowaweka kukusanya mapato hapo sokoni anawaamini kama wana shida au matatizo kuhusu soko wampigie simu.


Alisema yeye ndie mwenye maamuzi ya kuwaweka watu wa kukusanya mapato lengo la serikali ni kukusanya mapato na sio kelele za wakulima ho.
Mwisho

No comments:

Post a Comment