Photobucket

Wednesday, September 22, 2010

JE, TUFIKE MAHALI TUZIKUBALI HOJA ZA WAPINZANI?

NA KENETH GOLIAMA

Nimekuwa nikitafakali kwa makini sera za wapinzani nchini na kuona kama wanapotosha wananchi kwa kiasi kikubwa katika makombora yao kwa serikali kushindwa kuwapa elimu bure toka shule ya msingi hadi elimu ya juu.

Kwa kuona hilo nikatafakari kwa nini watanzania wengi wanashindwa kuhimili soko la afrika mashariki kimsingi nikatambua sio kuwa nauwezo wa kazi hapana ni kukosa elimu ya kuweza kushindana nao.

Nikatfakari kwa makini na kujiuliza watanzania wamekosa nini katika kupata elimu ya bure kama wakoloni walivyowapa wazazi wetu elimu bure hadi leo wao wanapinga maendeleo ya kutoa elimu bure kwa wananchi wa Tanzania wa sasa?.

Ukilinganisha Tanzania ni ya Tatu kimifugo Afrika na tena ni nchi maskini kupindukia ukilinganisha na nchi zisizo na mifugo Afrika jibu hakuna .

Tanzania imekuwa na rasilimali za kupindukia na zingine tunalalia wenyewe tukiendelea kulaumu kuwa sisi ni maskini huku tukiwaachia wenye elimu ya kutupita kuja kuchukua mali zetu na kwenda kuziuza nje ya nchi na wao kupata fedha nyingi zinazowafanya watoto wao wasome bure.

Kimsingi hakuna kuwadanganya wananchi wa Tanzania kuwa watanzania hawaezi kusoma bure kwani ni fedha ndogo sana wananfunzi wa Tanzania wanalipa katika elimu ya sekondari hadi kidato cha sita ambazo zinaweza kufutwa tu.

Sisemi haliwezekani maana kinachofutwa ni ada na michango ambayo haina msingi na kikwazo kwa wananchi wengi wa Tanzania ambao wanashindwa kupeleka wanafunzi wao shuleni.

Tujiulize anayepinga kusoma wanafunzi bure anauwezo gani na asiyepinga anauwezo gani ndipo tutapata jibu kuwa watanzania lazima tukubali kuwa elimu ya bure si kwa wachache bali ni kwa sisi watanzania tusiokuwa na uwezo.

Nchi yetu imefanikiwa kuwa na maliasili nyingi kama Madini, Mbuga za wanyama,Mito mingi yenye kila aina ya vitega uchumi kama samaki nyingi zinazofaidisha watu wasio watanzania na sisi kula vichwa tu na mikia lazima watanzania Tuzinduke.

“Kauli ya Tanzania bila elimu ya kulipia inawezekana kabisa” hii kauli lazima tuikubali kwa nguvu kubwa maana wanaosoma ni watoto watu wachache wenye uwezo hivyo tukikubali kuendelea na imani potofu ya wachache wao tutashindwa katika kila kitu.
Watoto wetu wamekuwa wakiandamana kwa mafungu ya Elimu ya vyuo vikuu lakini serikali haisemi chochote hii nikuonesha wachache wetu wasome ili watanznia wengi wasijue mali ganiinawafaa watanzania waweze kunufaika.

Kiwango wanacho lipa watoto wetu katika elimu yetu ni kidogo sana ambacho hata kikifutwa hakuna tija ya kusema uchumi utayumba bali uchumi utaimarika zaidi kwani wengi wetu watakuwa wamesoma hivyo kuweza kujiendeleza wenyewe.
Migodi ni mngi sana hivi tukiwazuia wawekezaji kuchimba bure miaka wanayopewa mitano nani anapata hasara wazungu watanzania wenyewe.

Kuna maswali mengi watanzania hawajapata majibu hivyo wanaburutwa tuu ilimradi siku zinaenda hii ni hatari kwa taifa letu kwani vitu vinapanda bei lakini hatusikii uchumi unapanda bali uanshuka zaidi viongozi kaeni chini tuambieni watanzania.

Watanzania wengi wanamkumbuka hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere kwani wote waliosoma nao walitumia mali za Tanzania kusoma bure bila buguza yeyote iweje kwa watanzania wa sasa?. watanazia wanataka kujua.

Wote waliosoma enzi za mwalimu walisoma bure wakapata elimu bora bila hata ya kuwepo wachimba madini wengi,wavuvi wengi, wawekezaji wengi,watalii wengi lakini leo kila sekta kumesheheni pesa lakini matumizi makubwa bila maendeleo bora.
Hivyo vyote havikuwepo lakini sasa kunakila aina ya watalii waekezaji viwanda vikubwa vinavyoingiza mali nyingi lakini mapato yake yanaishia kuwajali wa wachache na kuacha asilimia 75 ya watanzinia wanaosoma vijijini kwa hali ngumu kushindwa kusaisiwa hapa lazima serikali iangalie upya na wananchi wa Tanzania kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia watanzania wote na sio wachache.

Wanaopinga kusema watanzania hawapaswi kusoma bure aende mahali panapofanya maendeleo yamkubali mtanzania na kujisifu kwa watanzania kuwa amefanya jema ili tumhoji na sio kukurupuka tu na kusema watanzania hawapaswi kusoma bure.
Nina kubali kuwa nchi masikini inaongozwa na watu masikini waliofirisika katika kuleta maendeleo kwa wengi na badala yake kuleta maendeleo kwa wachache.

Siwatukani viongozi bali tunataka watu wenye uchungu na watanzania kwakuwa ndio wazawa wa mali zote zinazotoka hapa nchini kwa kila sehemu ya Tanzania watu wanalalia madini kwanini kila sehemu wasinufaike na madini.

Lazima tukae chni tubuni jinsi ya kuwaibia watanzania maana ukitaka mtanzania kushindana kwa kila kitu tumpe elimu ambayo ndio mkombozi wake kujua wapi anaibiwa na wapi haibiwi hapo tutaamini kuwa kile tulichonacho tumekifaidi.

Kilimo cha watanzania kimekuwa ndio uti wa mgongo kwao lakini hakuna chochote wanachokifaidi kutokana na ugharama wa bidhaa has pembe jeo ambazo wachache wao wanajisifu lazima tuwakemee kabisa kuwa wametuletea mzigo zaidi.

Sijaona mtanzania wa kijijini ambaye anauwezo wa kununua Powetiller hata kama wengi wao wakichanga 20 uwezo huo hawana ndio tuseme tumeinua kilimo lazima tukatae na Tuseme kilimo bila kufuta ushuru wa Pembejeo inawezekana
Tuangalie mapinduzi ya kijani na kilimo enzi za zamani huko ulaya ambayo yamekuwa msaada mkubwa wa maendeleo katika Tanzania, yalitokana kushirikiana kati ya Viwanda vya Mbolea na kilimo ndipo wakawa matajiri wa maendeleo ya maisha kwao kwa nini isiwe Tanzania.


Jambo si kusifu Ulaya kwa kutumia maliasili za Watanzania kusomesha watoto wao bure nasi bali inatakiwa kujiuliza chanzo chetu cha umaskini ni nini kama sio sisi wenyewe kutojua mchawi wetu nininani.

Mwisho

No comments:

Post a Comment