Wednesday, August 18, 2010
MICHUANO YA COPA COCA COLA YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI MBEYA
Na Chuma Amosy, Mbeya
Jumla ya timu Nane zikiwemo Shule tano za Sekondari naTatu za vituo vya Mitaani zimeanza michuano ya Copa coca cola ya vijana walio chini ya Umri wa miaka 17 katika Uwanja wa Sokoine mwishoni mwa wiki iliyopita Jijini hapa.
Akiongea na MwanaSpoti Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Jijini Mbeya (MUFA) John Gondwe alisema madhumuni ya kuwa michuano hiyo ni kuunda timu ya Jiji itakayocheza na timu nyingine za wilaya ili kupata timu moja ya mkoa wa Mbeya ambayo itashiriki Copa Coca Cola Taifa.
Pia alizitaja timu ambazo zinashiriki michuano hiyo kuwa ni Shule za Sekondari za St. Aggrey, Samora, Sinde, Meta, na Iganzo, kwa upande wa vituo vya mitaani alivitaja kuwa ni Mbeya Foundation, Mbaspo na Foysa.
MUFA ilitoa ratiba ya mitanange hiyo iliyoanza rasmi Jumamosi kwa kuzikutanisha timu za Mbaspo na Foysa(wapinzani wa jadi) na Mbeya Foundation ikikutana na St. Aggrey.
Katika mitanange hiyo ya ufunguzi Mbaspo iliikung’uta Foysa kwa jumla ya mabao matatu kwa moja huku St. Aggrey ikiigaraza Mbeya Foundation kwa bao moja kwa ubuyu.
Michuano ya Copa Coca Cola mwaka huu inafanyika nchini kote kwa madhumuni ya kusaka vipaja ambavyo hapo baadaye vitatengeneza timu ya taifa.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment