Photobucket

Saturday, April 3, 2010

HATUTA KUSAHAU SIMBA WA VITA

Na Johnson Jabir
MBEYA,

TANZANIAWaziri mkuu wa zamani wa Tanzania Rashid Mfaume Kawawa amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili alikolazwa jana kwa matibabu.

Kawawa atakumbukwa kama “Simba wa Vita” katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika ambapo Desemba 9, 1961 walipata kutoka kwa Mwingereza akiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Mara baada ya uhuru akawa Makamu wa Rais wa kwanza katika serikali ya Tanganyika.

Rashid Mfaume Kawawa alizaliwa tarehe 27, 1926 katika kijiji cha Matepwende,wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma.Alianza elimu yake ya Msingi huko Liwale Lindi mnamo mwaka 1941 na kuendelea na masomo ya sekondari ya Dar es Salaam.

Wadhifa wa kuwa Waziri mkuu wa Tanzania aliupata tarehe 22 Januari 1961 hadi Februari 13,1977 wakati huo akamwachia Edward Moringe Sokoine na baadaye alikuja kuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) MUNGU AWAFARIJI WAFIWA AMEN

No comments:

Post a Comment